Tuesday, January 26, 2010

Marekani yasitisha ufadhili wa elimu Kenya



Marekani imesitisha ufadhili wa dola millioni saba kwa mpango wa elimu ya bure kwa shule za msingi nchini Kenya.
Balozi wa marekani nchini Kenya Michael Ranneberger amesema ufadhili huo utasitishwa hadi pale madai ya ufisadi katika wizara ya elimu yatakapochunguzwa.
Hatua marekani kusimamisha ufadhili huo imechukuliwa mwezi mmoja baada ya serikali ya Uingereza kuondoa ufadhili wake kwa sekta hiyo ya elimu.
Balozi Ranneberger amesisitiza kuwa ni lazima mpango mzima wa elimu ya bure nchini Kenya ufanyiwe uchunguzi.
Marekani imekuwa ikishinikiza serikali ya Kenya kutekeleza mabadiliko.
http://www.bbc.co.uk/swahili

1 comment:

  1. Uongozi unadharau maoni ya wafanyakazi waendeshaji hasa wanapoongelea ..... Ufdhili utolewe kwa vikundi visivyokuwa na uwezo au makabila yenye ...... Malalamiko

    ReplyDelete