Tuesday, February 2, 2010

How Is Cancer Diagnosed?

The earlier cancer is diagnosed and treated, the better the chance of its being cured. Some types of cancer -- such as those of the skin, breast, mouth, testicles, prostate, and rectum -- may be detected by routine self-examination or other screening measures before the symptoms become serious. Most cases of cancer are detected and diagnosed after a tumor can be felt or when other symptoms develop. In a few cases cancer is diagnosed incidentally as a result of evaluating or treating other medical conditions.



Diagnosis begins with a thorough physical examination and a complete medical history. Lab studies of blood, urine, and stool can detect abnormalities that may indicate cancer. When a tumor is suspected, imaging tests such as X-rays, computed tomography (CT), magnetic resonance imaging (MRI), ultrasound, and fiberoptic scope examinations help doctors determine its location and size. To confirm the cancer diagnosis, a biopsy is performed: A tissue sample is surgically removed from the suspected malignancy and studied under a microscope to check for cancer cells.

Friday, January 29, 2010

LIBRARY Of LOVE



It is an innate desire of human beings to look attractive regardless of the hair type they have. Each ethnic race has its own standards of beautiful hair.

Mere presence of some beautiful hair strands on the scalp is of not much significance if not with coupled with some healthy and voluminous hair to match. You can have both the beauty and quantity if you follow some faster hair growth tips.

Growth of healthy hair largely depends on its normal healthy
functioning and structure. The hair structure is divided into
two parts - the non living part that is projected
out of the skin of the scalp and the other living part...

Click to read more ...

Wednesday, January 27, 2010

LIBRARY LOVE

Ni yapi maoni yako leo????    ?   Library For LOVE










Tuesday, January 26, 2010

Marekani yasitisha ufadhili wa elimu Kenya



Marekani imesitisha ufadhili wa dola millioni saba kwa mpango wa elimu ya bure kwa shule za msingi nchini Kenya.
Balozi wa marekani nchini Kenya Michael Ranneberger amesema ufadhili huo utasitishwa hadi pale madai ya ufisadi katika wizara ya elimu yatakapochunguzwa.
Hatua marekani kusimamisha ufadhili huo imechukuliwa mwezi mmoja baada ya serikali ya Uingereza kuondoa ufadhili wake kwa sekta hiyo ya elimu.
Balozi Ranneberger amesisitiza kuwa ni lazima mpango mzima wa elimu ya bure nchini Kenya ufanyiwe uchunguzi.
Marekani imekuwa ikishinikiza serikali ya Kenya kutekeleza mabadiliko.
http://www.bbc.co.uk/swahili

Marekani yakosoa utawala wa Nigeria




Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton amekosoa vikali utawala wa Nigeria kwa kutowajibikia majukumu yake vilivyo.
Bi Clinton amesema hali mbaya ya maisha nchini Nigeria imesababisha wananchi wengi na hasa vijana kuhisi kwamba wametengwa na sasa wamekuwa walengwa wa makundi ya kigaidi ambayo yanawasajili na kuanza kuwapa mafunzo ya itikadi kali.
Amezungumzia ongezeko la machafuko na uasi nchini Nigeria na kisa cha raia wa Nigeria Umar Farouk Abdulmutallab, ambaye anadaiwa kuhusika katika jaribio la kuidungua ndege katika anga za marekani mnamo siku ya krismasi.
Bi Clinton na Rais Barack Obama wameweka mbele kampeini ya kuwezesha utawala bora barani Afrika katika agenda yao.
http://www.bbc.co.uk/swahili
Creative Commons License
jAim Tanzania by Innovate,Stability & Services is licensed under a Creative Commons Attribution 3.0 United States License.
Based on a work at jaimtz.blogspot.com.
Permissions beyond the scope of this license may be available at http://jhamaro.wordpress.com/.

Monday, January 25, 2010

Who Else!

DJ JD SASA KUSIKIKA RADIO TIMES FM KATIKA KIPINDI CHA BLUST 100.5

John Dilinga (DJ JD) akisani mkataba wa kuitumikia Radio Times FM katika kipindi cha BLUST 100.5, anayemtazama ni Meneja vipindi wa Radio Times FM Scholastica Mazula.

DJ mkongwe nchini John Dilinga maarufu DJ JD amesaini leo mkataba na Radio Times FM tayari kuanza kuunguruma kupitia masafa ya 100.5.DJ JD ambaye inasadikia ndiye mkali na mtundu nchini Tanzania katika kuichezea Dj mashine na uchangaji wa muziki atakuwa akiendesha kipindi cha BLUST 100.5 kila siku kuanzia saa 10:00 jioni hadi saa 1:00 jioni, akitangaza na kumix mziki mwenyewe.Akizungumza na viwanjani DJ JD amesema kwamba wapenzi wa aina ya uchangaji muziki wake na wasikilizaji wa Radio Times FM wajiandae kupata burudani ambayo wameikosa kwa muda mrefu.DJ JD amesema wanaodhani kwamba uwezo wake umeshuka, wafute kabisa mawazo hayo na wakitaka kuthibitisha basi wasikilize Radio Times FM 100.5 na watathibisha kile ambacho wanakifikiria.DJ JD ni moja wa ma DJ na Watangazaji waliotoa mchango mkubwa katika kuunyanyua muziki wa kizazi kipya yaani Bongofleva.

FIFII MOTO NI MOTO KWELI ONA JAMAA ANAVYOUNGUA!!

Msanii mahiri wa miondoko ya Chakacha kutoka Nairobi Kenya Fifi Moto akimpagawisha shabiki wake kwa namna ya kipekee kabisa,kwenye onesho la taarab la kufungua mwaka lililofanyika usiku wa kuamkia juzi pale Traveltine Magomeni jijini Dar,Onyesho hilo ambalo lilifana sana liliandaliwa na kampuni ya Manywele Entertainment.

Waliomuua rais Kabila waachiliwe!!

Askofu Laurent Monsengwo Pasinya.

Askofu mkuu wa jimbo la Kinshasa Laurent Monsengwo Pasinya, ametaka kuwepo uchunguzi zaidi dhidi ya tuhuma zinazowakabili washukiwa wa mauaji ya rais wa zamani Laurent Desire Kabila. Amesema watuhumiwa hao huenda walihukumiwa kimakosa na kutaka wapewe msamaha wa rais na kuachiliwa huru.
Ujumbe huu umetolewa katika kumbukumbu za miaka tisa tangu rais huyo kuawa mnamo Januari mwaka 2001 na mlinzi wake wa karibu. Mtu huyo na wengine 30 walihukumiwa kifungo cha kifo na mahakama ya kijeshi.
Hata hivyo wengi serikalini ikiwa ni pamoja na washiriki wa karibu wa rais huyo wamepinga wito wa kuachiliwa huru kwa washukiwa hao wakisema kuwa watu hao wanafaa kuhudumia kifungo chao.
Hii ni mara ya kwanza msimamo kama huu unachukuliwa na kiongozi wa ngazi ya juu katika dhehebu katholiki lenye waumini wengi nchini humo http://www.bbcswahili.com/ .

Monday, January 25, 2010

VYAMA VYA SIASA VYAFUTIWA USAJILI WA MUDA!!

Msajiri wa vyama vya siasa John Tendwa.



Na Veronica Kazimoto – MAELEZO

Chama cha Peoples Democratic Movement ambacho mwenyekiti wake ni Joseph Minja kimefutiwa usajili wake wa muda kwa kushindwa kutimiza masharti ya kisheria.
Taarifa kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa zinasema chama hicho kimefutiwa usajili kwa kutotekeleza sheria namba 5 ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 inayosema kuwa ni lazima chama kiwe na wanachama 200 au zaidi.
Kwa mujibu wa sheria hiyo, chama cha Peoples Democratic Movement hakikuweza kufikisha idadi hiyo ya wanachama, hivyo msajili wa vyama vya siasa ameamua kukifutia usajili wake wa muda.
Wakati huo huo chama cha Democratic National Congress (DNC) kimekataliwa na msajili wa vya siasa kuongezewa muda wa usajili kwa mara ya tatu na hivyo kufutiwa usajili wake wa muda.
Taarifa ya msajili wa vyama vya sisa imebainisha kuwa, sheria ya vyama vya siasa namba 5 ya mwaka 1992 kifungu cha 8 (4) inaeleza kwamba usajili wa muda wa chama chochote utakoma kuendelea baada ya kuisha muda wa siku 180
Kwa mujibu wa sheria hiyo, chama cha DNC kimepitiliza muda huo na tayali kilishawahi kuongezewa muda mara mbili. Chama hicho kilisajiliwa mwaka 2008 na mpaka sasa takribani mwaka mzima umekwishapita.

TUME YA UCHAGUZI YASEMA MWISHO WA KUPOKEA MAOMBI YA KUGAWA MAJIMBO NI FEBRUARI 28/2010!!

Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Omar Makungu akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutani wa ofisi za tume ya uchaguzi wakati viongozi hao walipotangaza rasmi halmashauri za Wilaya na Mikoa kupeleka maombi ya kugawa majimbo ya uchaguzi kwa kuzingatia vigezo vilivyoainishwa na tume hiyo kwa mikoa na Wilaya zinazoomba kugawa majimbo yao.
Amesema mwisho wa kupeleka maombi hayo itakuwa februari 28 2010 na baada ya hapo tume hiyo itapitia maombi hayo na kuona ni mikoa na wilaya gani zimekidhi na kufuata maelekezo ya tume hiyo ili majimbo yao yaweze kugawanywa, gharama halisi itakayotumika ktika shughuli za kugawa majimbo ni shilingiMilioni 50.
Akizungumzia gharama za uchaguzi wa mwaka huu Mwenyekiti wa tume hiyo Rajabu Kiravu amesema gharama hizo zimegawanyika katika awamu tatu ambapo uboreshaji wa Dafrtari la wapiga kura awamu ya kwanza uligharimu shilingi Bilioni 27 na awamu ya pili uligharimu shilingi bilioni 42 na uchaguzi mkuu utagharimu shilingi bilioni 64.
Tanzania inatarajiwa kufanya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani hapo baadae mwaka huu na vyama mbalimbali viko katika pilikapilika za kujiandaa na uchaguzi huo baada ya awamu ya kwanza ya kipindi cha miaka mitano ya Rais Jakaya Kikwete kumalizika, aliye kulia katika picha ni mwenyekiti wa tume ya uchaguzi (NEC) Rajabu Kiravu.

Sunday, January 24, 2010

Muujiza baada ya uokozi Haiti kusimamishwa!!

Baada ya siku 11 tangu tetemeko la ardhi kusababisha maafa makubwa kisiwani Haiti wengi walipigwa na butwaa wakati mwanamume mmoja aliokolewa kwenye maporomoko ya hoteli moja mjini Port-au-Prince.
Awali serikali ya Haiti ilikata tamaa na rasmi kusimamisha juhudi zozote za kuwatafuta manusura.
Walioshuhudia walibubujikwa na furaha na kupiga makofi wakati Wismond Exantus mwenye umri wa miaka 24 aliponyanyuliwa kutoka kwa vifusi vya hoteli ya Napoli.
Aliwaambia waandishi wa habari kwamba kwa siku hizo zote alitegemea soda na vitafunio vidogo vidogo.
“Nilikuwa nitumia Coca-Cola na vitu vingine vidogo vidogo,” alisimulia Exantus.
“Kila siku nilikuwa na matumaini ya kwamba nitanusurika.”
Waokozi kutoka Ugiriki, Ufaransa na Marekani walitumia zaidi ya saa mbili unusu wakijaribu kumwokoa.
Mmoja wao kutoka Ufaransa, Luteni Kanali Christophe Renou alitaja tukio hilo kama “muujiza”. http://www.bbcswahili.com/

YANGA YAIGEUZIA MKUKI WA SUMU MANYEMA RANGERS!!

Beki wa Yanga, Shadrack Nsajigwa (kulia) akimkaba mshambuliaji wa Manyema, Ally Mohamed ‘Gaucho’.


Timu ya Yanga ya jijini Dar es salaam imeifunga timu nyepesi ya Manyema Rangers pia ya Dar es salaam magoli 3-1 katika mfurulizo wa michezo ya ligi kuu ya Vodacom inayoendelea katika viwanja mbalimbali hapa nchini.
Mchezo huo ulikuwa wa upande mmoja timu ya Yanga imekosa magoli mengi kutokana na mashambulizi iliyoyafanya kwenye goli la timu ya Manyema ingeweza kuibuka na ushindi mkubwa zaidi kama wachezaji wake wangetumia vyema nafasi walizozipata langoni mwa Manyema Rangers .
Magoli ya yanga yamefungwa na mchezaji wake machachari Mrisho Ngasa aliyefunga magoli mawili kwenye kipindi cha kwanza cha mchezo huo na kuongeza goli la tatu katika kipindi cha pili huku timu hiyo ikiendelea kulisakama lango la timu ya Manyema Rangers.
Manyema Rangers walijipatia goli la kufutia machozi katika kipindi cha pili lililofungwa na mchezaji wake Ally Mohamed hivyo kuzifanya timu hizo zitoke uwanjani kwa magoli 3 kwa timu ya Yanga na goli 1 kwa timu ya Manyema Rangers mara baada ya filimbi ya mwisho wa mchezo huo kupulizwa.

Mhubiri wa Jamaica awasili nyumbani!!

Sheikh Abdullah al-Faisal

Mhubiri wa kiislam aliyefukuzwa kutoka Kenya kutokana na sababu za kuwa tishio kwa usalama, amewasili nchini kwao, Jamaica, ambako amehojiwa na polisi.
Maafisa walisema mhubiri huyo, Abdullah al-Faisal, hakuvunja sheria yeyoye nchini Jamaica, lakini polisi walitaka kujua ni wapi wanaweza kumpata.
Bw al-Faisal, ambaye alitumikia kifungo che jela nchini Uingereza kwa kuchochea mauaji, amaearifiwa kuwafahamisha polisi nchini Jamaica kuwa safari yake ya ndege ya siku mbili kutoka Kenya, iligharimu dola nusu milioni.
Kwa uchache watu watano waliuwawa mjini Nairobi, baada ya polisi kuwafyatulia risasi waandamanaji waliokuwa wakirusha mawe, ambao walikuwa wanadai kuachiliwa huru kwa Bw al-Faisal.
Serikali ya Kenya ilimkamata Bw al-Faisal mwishoni mwa mwezi uliopita mjini Mombasa kwa madai ya kukiuka kanuni na uhamiaji.

Vodacom yazindua kampeni ya kuchangia waathirika wa maafa yanayotokana na majanga mbalimbali nchini!!

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare(katikati) akizungumza na Waandishi wa habari leo asubuhi kabla ya uzinduzi wa kampeni ijulikanayo kama Vodafone Red Alert,inayoendeshwa na kampuni ya Vodacom Tanzania.Kampeni hiyo inalenga kuwahamasisha wateja wa Vodacom kuwachangia Watanzania waliopatwa na maafa kwa kutuma neno MAAFA kwenda namba 15599,kila ujumbe mmoja utatozwa shilingi 250.alieyakaa kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Meja Jenerali mstaafu Bakari Shabani na kulia ni Mkurugenzi wa Uhusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba
Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Meja Jenerali mstaafu Bakari Shaban, akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom wanaohusika waliojitolea kusaidia jamii wakati wa maafa, Voda Heroes wakiwa katika uzinduzi wa kampeni ya kusaidia wahanga wa maafa mbalimbali hapa nchini.


Vodacom Tanzania imezindua kampeni ya kusaidia waliofikwa na maafa, na kupitia kampeni hiyo, wateja wa Vodacom sasa wanaweza kutoa michango yao kwa wahanga wa majanga hayo.
Akizindua kampeni hiyo leo asubuhi , Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Bw Dietlof Mare alisema kampeni hiyo ni muhimu katika kuyarejesha katika hali ya kawaida maisha ya Watanzania walioathiriwa na maafa katika sehemu mbalimbali za nchi.
Aliwataka wateja wa Vodacom na Watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika kampeni hiyo ili waweze kuwasaidia waathirika wa majanga hayo.
Ili kuwachangia wahanga, wateja wa Vodacom wanapaswa kutuma ujumbe wenye neno MAAFA au REDALERT kwenda namba 15599, na ujumbe huo wa mchango unagharimu Sh. 250 pamoja na VAT, mteja anaweza kutuma mara nyingi kadri awezavyo.
Kampeni itakuwa ni ya wiki moja kuanzia tarehe 24 Januari mpaka tarehe 1 Februari mwaka huu.
Alisisitiza kuwa bila ya ushirikiano wa wateja wapatao milioni saba wa Vodacom Tanzania zoezi hili halitafanikiwa na hivyo kuwaomba wateja wachangie kwa wingi mfuko huo kwa njia ya kutuma ujumbe mfupi.
Bw Mare alivishukuru vyombo vya habari nchini kwa kutoa ushirikiano wao kwenye kampeni hii na kuomba ushirikiano wa namna hiyo udumu kwa manufaa ya Watanzania.
Nae Mkurugenzi wa Kitengo cha Mfuko wa Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Meja Jenerali Mstaafu Bakari Shabani, alipongeza Vodacom kwa kuanzisha kampeni hii na kuwataka watanzania kwa ujumla kuchangia mfuko huo.
Alisema kwamba siku zote panapotokea majanga mtu wa kwanza anayepaswa kujisaidia ni mwathirika mwenyewe kabla ya kungoja msaada kutoka nje.
Alitoa wito kwa makampuni mbalimbali hata kama siyo ya simu kuwasawaidia waathirika wa majanga hapa nchini.
“Nawapongeza Vodacom Tanzania kwa kuanzisha mpango huu wa kusaidia Watanzania wenzao, nayaomba makampuni mengine nayo yajitokeze,”
Mkurugenzi wa Uhusiano wa Vodacom alisema mpango huo wa Vodafone Red Alert uko katika nchi 27 ambazo kampuni ya Vidafone ipo.
“Hivyo wajibu wetu ni kuwawezesha kwa teknolojia Watanzania wenyewe waweze kuchangia,” alisema.
Alisema kila mara yatakapotokea majanga, basi Vodafone Red Alert itakuwa ya kwanza kuanzisha kampeni ya Watanzania kuchangi,”

Saturday, January 23, 2010

SIMBA YAITUNGUA TIMU YA PRISON KWENYE UWAJA WA UHURU!!

Kutoka kushoto ni kocha wa timu ya Simba Patrick Phiri, Meneja Inocent Njovu na Amri Said kocha msaidizi wa timu hiyo wakifuatilia pambano katika ya timu yao na timu ya Prison kutoka mkoani mbeya.


Timu ya Simba ya jijini Dar es salsaam leo imeitungua timu ya magereza Prison kutoka mkoani Mbeya kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliozikutanisha timu hizo kwenye uwanja wa Uhuru maarufu kama (shamba la bibi).
Mchezo huo ulikuwa ni mkali lakini kama kawaida yake timu ya Simba ilionekana kutawala karibu kipindi chote cha kwanza cha mchezo huo na kufanya mashambulizi mengi katika lango la timu ya Prison, hata hivyo kazi nzuri ya golikipa wa timu hiyo ndiyo iliyoiokoa Prison.
Katika kipindi hicho cha kwanza simba ilifanikiwa kupata magoli kupitia wachezaji wake Mussa Hassani "Mgosi" aliyeifungia timu hiyo goli la kwanza huku mchezaji mwingine Nico Nyagawa akifunga goli la pili.
Katika kipindi cha pili timu ya Prison ilijitutumua na kujipatia goli la kwanza na la kufutia machozi kupitia kwa mchezaji wake Misango Magae, goli lililoipa nguvu timu hiyo na kushambulia lango la timu ya Simba mara kwa mara bila mafanikio.
Shujaa wa simba Mussa Hassan Mgosi aliwanyanyua mashabiki wake tena mara baada ya kukandamiza goli la tatu kwenye lango la Prison goli lililoifanya timu hiyo kunyong'onyea kabisa kimchezo, hata hivyo mara baada ya mchezo huo kocha wa Prison James Nestory amesema timu yake imefungwa kimchezo kwani timu ya Simba ilicheza vizuri, lakini pia wachezaji wake hawakuwa vizuri kimchezo kutokana na kuathirika kisaikolojia kwa sababu ya kupoteza michezo mingi ya ligi kuu ya Vodacom.

Bima ya mifugo yazinduliwa Kenya!

Mfumo mpya wa bima ambao utawapatia wafugaji fursa ya kuwalinda mifugo wao kutokana na ukame umezinduliwa kaskazini mwa Kenya.
Mpango huu unatumia tiknolojia ya satellite kuangalia hali ya malisho kwenye maeneo ya wafugaji.
Ardhi iliyo kavu kaskazini mwa Kenya mwaka jana ilikumbwa na ukame mbaya ambao ulisababisha vifo vya maelfu ya mifugo.
Kufikia sasa haikuwa rahisi barani Africa kutoa bima kwa mifugo katika maeneo ya vijijini.
Lakini sasa juhudi mpya zilizoanza kutumika mjini Marsabit, kaskazini mwa Kenya zinatoa matumaini wakati ukame unapokumba jamii za wafugaji.

MNUSO WA AROBAINI YA DJ YOUNG KIM JIJINI DAR ES SALAAM!

Ndugu jamaa na marafiki wa Marehemu Abdulhakhim Magomelo (DJ Young Kim) aliyefariki siku arobaini zilizopita jijini Dar es salaam kwa matatizo ya moyo katika Hospitali ya Saint Monica walijitokeza nyumbani kwake katika hitma ya arobaini iliyofanyika mchana huu katika mtaa wa mkwepu, Dj Young Kim alikuwa kipenzi cha watu wengi na hii ilijidhijirisha wakati wa mazishi yake ambapo watu wengi maarufu na wadau wa muziki walijitokeza ili kumzika Dj huyo wa zamani katika makaburi ya Kisutu, mbali ya kuwa Dj Maarufu hapa nchini enzi hizo, Dj Youg Kim anakumbukwa kwa mengi aliyoyafanya katika muziki kama vile kuandaa mashindano mablimbali ya madansa na mashindano ya marapa wa muziki wa hiphop nchini Tanzania tamasha lililojulikana kama (Yo Rap Bonanza).
Ndugu jama na marafiki wakipata mnuso.

Adebayor arejea baada ya shambulio!

Mshambuliaji wa Manchester United na timu ya taifa ya Togo Emmanuel Adebayor.

Emmanuel Adebayor anatazamiwa kujiunga na kilabu yake ya Manchester City huku akiwa bado na msongo kufuatia shambulio dhidi ya timu ya taifa ya Togo wiki mbili zilizopita.
Timu hiyo ilikuwa ikielekea Angola kushiriki kwenye mashindano ya kombe la mataifa barani Afrika wakati iliposhambuliwa na waasi katika eneo la Cabinda.
Wachezaji kadha walijeruhiwa na mmoja wa wale waliopigwa risasi alifariki dunia akiwa mikononi mwa Adebayor.
Serikali ya Togo ilieleza kuchukizwa kwake kutokana na shambulio hilo na kuamuru timu ya taifa kutoshiriki katika mashindano hayo.
Adebayor alieleza jinsi kisa hicho kilikuwa kikimpa msongo, "ninatokwa na jasho kila siku. Nimepoteza hamu ya kula."
"Itanichukuwa muda kurejea uwanjani."

Friday, January 22, 2010

'HOPE FOR HAITI NOW' GLOBAL TELETHON LIVE ON DStv

This Saturday viewers in Africa can join a global audience raise money for ‘HOPE FOR HAITI NOW’ as DStv screens the emergency benefit concert, in response to the crisis in Haiti following the devastating earthquakes, live across the continent.

The global telethon will be aired live across the DStv bouquet on National Geographic Channel, MTV, MTV Base and VH1 on Saturday January 23, 2010.
‘HOPE FOR HAITI NOW’, the concert is a telethon partnership between MTV and George Clooney and will be broadcast live from New York and Los Angeles. The show includes performances from London, various celebrity appearances and live cross-overs to Haiti.George Clooney will be hosting in Los Angeles, Wyclef Jean hosts in New York and CNN's Anderson Cooper will be reporting from Haiti.The concert being broadcast in a two-hour telethon will air live on the following DStv channels; National Geographic Channel (channel 260), MTV (channel 321), MTV Base (channel 322) and VH1 (channel 323) on Saturday January 23 at 03:00 CAT.

Audiences can also tune in for E! Entertainment’s (channel 124) coverage at 21:30 CAT while the Style Network (channel 183 will be airing the event at 23:00 CAT.

Artists confirmed to perform include: Wyclef Jean, Bruce Springsteen, Jennifer Hudson, Mary J. Blige, Shakira, Madonna, Beyonce, Sting, Alicia Keys, Christina Aguilera, Dave Matthews, John Legend, Justin Timberlake, Stevie Wonder, Taylor Swift, Cold Play and group performances by Keith Urban, Kid Rock and Sheryl Crow, as well as Bono, The Edge, Jay-Z and Rihanna.Also putting in appearances are; Will Smith, Brad Pitt, Meryl Streep, Tom Hanks and Leonardo DiCaprio.The relief organisations that the proceeds of the telethon will be going to are: Oxfam America, Partners in Health, the Red Cross, UNICEF, Yele Haiti Foundation, The Clinton Bush Haiti Fund and the United Nations World Food Program.

WHO yakabidhi msaada Wizara ya afya na ustawi wa jamii!!

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mh.Prof David Mwakyusa akipokea vifaa vya dharura na upasuaji kutoka kwa mwakilishi wa Shirika la afya Duniani nchini Tanzania Dr. Martins Ovberedjo.Vifaa hivyo vina thamani ya shilingi milioni 153 za kitanzania,vifaa hivyo vitapelekwa kwenye wilaya za kanda nane nchini .Makabidhiano hayo yamefanyika wizara ya afya na ustawi wa jamii makao makuu jijini leo.

Banza, Jumbe kuipamba Twanga Januari 29!!

Ramadhan MasanjaBanza Stone.
WASANII nguli wa Tanzania, Ramadhan Masanja 'Banza Stone' na Fresh Jumbe anayefanya shughuli zake Marekani, wanatarajia kutia nakshi katika onyesho la bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta' litakalofanyika kwenye ukumbi wa Koyanga Night Park, Kiwalani, Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kampuni ya First Entertainment inayoandaa onyesho hilo, Victorian Nachenga 'Victor Buguruni', alisema Dar es Salaam jana kuwa Twanga Pepeta itafanya onyesho hilo Ijumaa ya Junuari 29, mwaka huu kuanzia saa 3 usiku kwa kiingilio cha sh. 5,000, huku Banza na Jumbe wakiwasindikiza.
Victorian alisema Twanga Pepeta pia itawapa mashabiki wao staili ya 'Sugua Kisigino' katika onyesho hilo ambalo pia ni sehemu ya 'kurudi nyumbani' kwenye ukumbi huo uliopo Kiwalani Kijiwe Samli.
Mkurugenzi huyo alisema onyesho hilo pia litapambwa na burudani kutoka kwa wasanii wengine watakaotangazwa baadaye.
Twanga Pepeta inayotamba na albamu ya 10 ya bendi hiyo, Mwana Dar es Salaam, itapiga nyimbo zake saba mpya zikiwamo Sumu ya Mapenzi uliotungwa na Khalid Chuma 'Chokoraa', Ubaya Aibu (Saulo John 'Ferguson'), Sitaki Tena (Saleh Kupaza), Nazi Haivunji Jiwe (Thabit Abdul).
Nyingine ni Rafiki Adui uliotungwa na Rogart Hega 'Katapila' na Shida Darasa na Mwana Dar es Salaam uliobeba jina la albamu, zilizotungwa na Charles Gabriel 'Chaz Baba'.

400,000 kuhamishwa nchini Haiti!

Serikali ya Haiti imesema kuwa itawahamisha zaidi ya waathiriwa laki nne kutoka mji mkuu wa Port Au Prince kufuatia tetemeko la ardhi la wiki iliyopita.
Waziri wa masuala ya ndani Paul Antoine Bien-Aimé amesema kuwa tayari mabasi yameandaliwa kuwasafirisha waathiriwa hao kutoka mji mkuu hadi vijijini kusini na kaskazini mwa nchi hiyo.
Serikali hiyo imesema kuwa takriban miili 75,000 imezikwa katika makaburi ya pamoja japo inaamini kuwa idadi ya waliofariki ni kubwa zaidi.
www.bbcswahili.com

DIAMOND MUSICA YAMCHOMOA MULEMULE KUTOKA FM ACADEMIA

Mkurugenzi msaidizi wa bendi ya Diamond Musica Perfect Kagisa katikati akiongea na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo wakati uongozi wa bendi hiyo ulipotangaza wanamuziki wake wapya watano waliojiunga na bendi hiyo hivi karibuni.
Perfect amesema wamemchukua mmoja wa wanamuziki nguli wa bendi pinzani ya FM Academia Mulemule au FBI ambaye atakuwa kiongozi wa bendi hiyo kwa sasa huku wakiwatwaa wanamuziki wengine wanne kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambao ni Kabongo Mamale, Sone Masamba, Guy Bonheur, Pirro Jazzo na Patien Losso ambaye anapiga gitaa la sollo.
Amesema wamedhamiria kufanya mambo makubwa kwa mwaka huu wa 2010 na ndiyo maana wameanza na kasi ya kuongeza wanamuziki ili kuimarisha kikosi chao cha uimbaji na unenguaji pia kwa upande wa wanaume "lakini pia tukaona tuimarishe upande wa gitaa la sollo kwa kumchukua huyu Patien Losso".
Amesema bendi hiyo inatarajia kuingia kambini januari 26 wiki ijayo kwa ajili ya kufanya mazoezi ya nyimbo mpya na kuunganisha wanenguaji katika kucheza staili mbalimbali zilizobuniwa kabla bendi hiyo haijaanza rasmi kufanya mambo yake ikiwa na wanamuziki wake wapya, wengine waliopo katika picha waliokaa kutoka kulia ni Kabongo Mamalee mwanamuziki, Juddy Moshi Mkurugezi wa bendi hiyo na kushoto ni Mulemule kiongozi wa bendi hiyo na Alan Mulumba kashama aliyeko mwisho.
Wanamuziki wa bendi hiyo wakionyesha vitu vyao mbele ya wanahabari mara baada ya mkutano.

TAARIFA YA KATIBU MKUU KULAANI MAUAJI YA WATOTO WAWILI YALIYOTOKEA WILAYANI NGORONGORO, ARUSHA!!.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Margareth Sitta
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto inakemea vikali mauaji ya watoto wawili Mpole John (13) na Faidika John (7) wote wa familia moja, ambao walikufa papo hapo baada ya Baba yao kuwapiga kwa kitu chenye ncha kali kwa madai kuwa, mke wake aliwazaa nje ya ndoa; tukio lililotokea katika Wilaya Ngorongoro Mkoani Arusha tarehe 17 Januari, 2010 asubuhi.
Wizara imepokea taarifa ya mauji ya watoto hao kwa masikitiko makubwa maana matukio ya kikatili ya aina hii yanapotokea katika ngazi ya familia, yanarudisha nyuma kwa kiasi kikubwa juhudi za Serikali katika kuzuia na kutokomeza vitendo vya ukiukwaji wa Haki na Ustawi wa Mtoto. Aidha, mauaji haya yamewakosesha watoto haki yao ya msingi ya kuishi ambayo ni haki yao ya kikatiba na ni kitendo kinacho kinzana na Mikataba ya Kimataifa ya Haki na Ustawi wa Mtoto ambayo imeridhiwa na nchi yetu.
Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto inahimiza jamii kubadilika na kuhakikisha kuwa familia ambayo ndiyo kitovu cha wanajamii panakuwa ni mahala salama penye upendo amani na mshikamano miongoni mwa wanafamilia; na kuwapatia watoto haki zao muhimu ikiwemo haki ya kuishi, kulindwa, kutobaguliwa na kuendelezwa.
Wizara inatoa rambirambi kwa mama, ndugu na jamaa wa watoto Mpole John na Faidika John waliouwawa maana maisha yao yamekatishwa; kwani wamempokonywa haki yao ya kuishi katika umri mchanga kwa kufanyiwa ukatili wa kinyama. Wizara inawaomba wawe wavumilivu katika kipindi hiki cha majonzi mazito.

TISHIO LA MOTO TENA BRITISH COUNCIL, WAFANYAKAZI WATOKA BARUTI!

Wafanyakzi wa British Council wakiamuliwa kutoka nje ya jengo ambapo imearifiwa kuwa Kuna tishio la kulipuka kwa moto katika jengo la ofisi hizo jijini Dar es salaam asubuhi hii mpaka sasa wafanyakazi wa tasisi hiyo ya Uingereza wametolewa nje ya ofisi ili kuchukua tahadhari ya usalama wao kama moto utaanza kuwaka, wanausalama wa kikosi cha kuzima moto cha kampuni binafsi ya ulizi Ultimate Security tayari wako hapo wakikagua huku na kule ili kubaini kama ni wapi kwenye hitilafu, king'ola kimekuwa kikilia kwa muda kitu kinachoashiria kuwa kuna tishio la moto katika jengo hilo.

Thursday, January 21, 2010

Jaji Mstaafu Mark Bomani awa mwenyekiti wa EITI

Mwenyekiti wa Kamati ya kusimamia utekelezaji wa Majukumu ya Mpango wa Tansia ua Uziduaji (EITI -Extractive Industries Transparency Initiative ) Jaji Mstaafu Mark Bomani (kushoto) akiongea na Wajumbe wa Kamati yake ya EITI baada ya kutambulishwa. na Naibu Waziri wa Nashati na Madini Adam Malima (kulia) kwa wajumbe wa kamati hiyo jijini leo.. Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO..
Kamishna wa Madini katika Wizara ya Nishati na Madini Dr. Peter Dalali Kafumo (kulia) akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya kusimamia utekelezaji wa Majukumu ya Mpango wa Tansia ya Uziduaji.(EITI - Extractive Industries Transparency Initiative) Jaji Mstaafu Mark Bomani jijini leo katika hafla ya utambulisho kwa Mwenyekiti wa EITI kwa wajumbe wa Kamati hiyo.

FRANCIS CHEKA NA MBWANA MATUMLA WAPATA MENEJA!!

Mabondia Francis Cheka kushoto na Mbwana Matumla kulia wakiwa na Meneja wao Juma Ndabile mara baada ya meneja huyo kuongea na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa idara ya habari maelezo juu ya mkataba wa mwaka mmoja aliosaini na mabondia hao ili kufanya nao kazi, meneja huyo atakuwa na jukumu la kuwatafutia mabondia walimu kwa ajili ya mafunzo na kuwatafutia mapambano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi pamoja na kuingia mikataba mbalimbali ya mapambano na udhamini.

ASKOFU METHODIUS KILAINI KUAGWA JANUARI 31!!

Katibu wa kamati ya maadalizi ya kumuaga Askofu Methodius Kilaini aliyekuwa msaidiza wa Kadinali Polcarp Pengo jimbo kuu la Dar es salaam aliyehama kikazi na kuwa Askufu wa Jimbo la Bukoba Bw. Jovin Bantulaki akizungumza na wanahabari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo kuhusu sherehe za kumuaga askofu huyo zitakazofanyika januari 31 baraza la Maaskofu kurasini jijini Dar es salaam, katibu huyo amewakaribisha watu mbalimbali waliowahi kusoma na kufanya kazi na mtumishi huyo wa mungu ili waweze kujumuika pamoja katika kumuaga.

HALI HALISI YA MAFURIKO YA KILOSA!

Hii ndiyo hali halisi ya Kilosa makazi mengi ya watu bado yamezingirwa na maji shughuli nyingi bado haziendi vizuri kutokana na athari za mafuriko hayo yaliosababisha hasara ya uharibifu wa mali na maisha ya watu ambapo kwa sehemu kubwa wananchi hao wanaishi kwa shida . picha hii imepigwa na Clarence Nanyaro wa Ofisi ya makamu wa Rais.

OFISI YA WAZIRI MKUU YAKABIDHI MICHANGO YA RAMBIRAMBI WA FAMILIA YA MAREHEMU MZEE RASHID KAWAWA!

Waziri wa Nchi ,Sera, Uratibu na Bunge Philip Marmo akimkabidhi kwa niaba ya ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Rehema Rashid Kawawa, mtoto wa marehemu Mzee Rashid Mfaume michango mbalimbali kutoka marafiki mbalimbali wakiwemo Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Mashirika, Taasisi na watu Binafsi. Zaidi ya shilingi milioni 24 ikiwa ni michango ya rambirambi zilikabidhiwa kwa familia ya marehemu Rashid Mfaume kawawa jana jioni.
(Piha na Aron Msigwa - MAELEZO).

Waziri wa Nchi ,Sera, Uratibu na Bunge Philip Marmo akitoa salam za pole kwa familia ya marehemu Rashid Mfaume Kawawa kwa niaba ya ofisi ya Waziri Mkuu ambayo iliratibu mazishi ya marehemu mzee Rashid Kawawa jana jioni kijijini Madale jijini Dar es salaam.



Amnesty yatoa wito wa ukaguzi zaidi wa silaha Somalia!

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu, Amnesty International, linataka shughuli ya kuisaidia serikali ya mpito ya Somalia na silaha isimamishwe.
Shirika hilo la kutetea haki za binadamu limesema kuwa silaha zinazopelekewa serikali ya mpito ya Somalia, mara nyingi hutumika dhidi ya raia. Aidha, Amnesty International imesema kuwa mara nyingine silaha hizo badala ya kutumiwa na serikali huangukia mikono ya makundi yanayopinga serikali.
Nchi ya Somalia imewekewa vikwanzo vya kuingiza silaha nchini humo. Lakini, shirika la Umoja wa Mataifa lilitoaidhini kwa serikali hiyo ya mpito ambayo inakabiliana na wanamgambo wa kiislamu kupewa silaha.
Nchi ya Somalia imejaa silaha na kuna makundi mengi yamejihima kupigania mamlaka.
Lakini wakati jamii ya kimataifa inajaribu kuisaidia serikali hiyo hafifu ya Somalia, silaha zaidi zinaingizwa nchini humo.
Mwaka uliopita serikali ya Marekani ilipeleka tani 19 ya silaha Somalia.

Ziara ya Makamu wa Rais Dk. Ally Mohamed Shein Wilayani Kilosa!!

Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein akitoka kukagua moja kati ya mahema ambayo yatatumika kama makazi ya muda kwa wananchi wa Wilaya ya Kilosa katika eneo la Kimamba alipotembelea Wilaya hiyo jana kuangalia kiwango cha athari na misaada inayohitajika.
Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein akipata maelezo ya ujenzi wa makaazi ya muda toka kwa Mkuu wa wilaya ya kilosa Halima Dendegu katika eneo la Magomeni mjini Kilosa jana wakati Dk shein alipofanya ziara ya kuwatembelea waathirika wa mafuriko ambayo yameikumba wilaya ya Kilosa kutokana na mto Mkondoa kujaa maji ya mvua na kina chake kupungua.
(Picha na Clarence Nanyaro wa Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein akiwafariji baadhi ya waathirika wa Mafuriko yaliyoikumba wilaya ya Kilosa wakati alipowatembelea katika eneo la Magomeni jana ambako inajengwa kambi ya muda ya kuwasitiri wananchi hao ambao kwa sasa wamehifadhiwa katika ghala la kilichokuwa kiwanda cha mazulia Kilosa.

Baadhi ya Mitaa ya Mji wa Kilosa bado imezingirwa na maji kutokana na mafuriko yaliyoikumba wilaya hiyo na kufanya uharibifu mkubwa wa miundombinu pamoja na mali za wananchi na kupoteza maisha kwa baadhi ya wananchi.

Rais Kikwete azindua programmu ya Kilimo Kwanza Wilayani Maswa Mkoani Shinyanga!!

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi ufunguo wa trekta ya mkopo Bwana Abdallah Thani,Mkulima wa Lalago wilayani Maswa wakati wa hafla ya uzinduzi wa programu ya Kilimo kwanza wilayani Maswa, Mkoani Shinyanga. Katika hafla hiyo matrekta kadhaa na power tillers zilikabidhiwa kwa wakulima kwa mkopo nafuu chini ya ufadhilki wa kampuni ya Al Adawi.
(picha na Freddy Maro wa Ikulu)


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia wananfunzi wa shule mpya ya Sekondari ya Masengwa katika wilaya ya Shinyanga wakifanya jaribio la kisayansi muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuifungua rasmi shule hiyo jana mchana.Shule hiyo imejengwa kwa ufadhili wa kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Barrick Gold inayomiliki mgodi wa Buzwagi mkoani Shinyanga.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua mojawapo ya darasa katika shule mpya ya sekondari ya Masengwa wilayani Shinyanga muda mfupi baada ya kuifungua rasmi jana mchana.

Mwenyekiti Mstaafu wa UWT Mkoa wa Shinyanga na mmoja wa waasisi wa CCM Bi. Jennyrose Kigola akimsalimia kwa hisia Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kuwasili ikulu ndogo mkoani Shinyanga jana .Kushoto pembeni ya Rais ni mke wa Rais Mama Salma Kikwete.

Wednesday, January 20, 2010

Tumedhibiti ghasia,asema mkuu wa jeshi Nigeria!

Wanajeshi wa Nigeria wakiwa na silaha zao wakati wa machafuko ya jimbo la Delta nchini humo.

Jeshi la Nigeria limesema limechukua udhibiti wa mji wa Jos,ambapo mapigano ya hivi karibuni kati ya waislamu na wakristo yalisababisha vifo vya watu kadhaa.
Luteni Kanali Shekari Galadima ameiambia BBC kuwa mji "uko shwari" wakati jeshi likihakikisha kuwa amri ya kutotoka nje kwa muda wa saa 24 inatekelezwa. Amesisitiza kuwa hakutakuwa na ghasia tena.
Lakini mwandishi wa BBC katika eneo hilo anasema ghasia sasa zimezidi hadi katika mji wa Pankshin, kilomita 100 kutoka Jos.
Makundi ya kutetea haki za binaadamu yanasema takriban watu 200 wanaaminika kufariki dunia tangu Jumapili.
Mji wa Jos umekumbwa na mapigano ya kidini kwa takriban muongo mmoja uliopita. http://www.bbcswahili.com/

Magambo ya K-Mondo yaruka kwenye video!

Bendi ya muziki wa dansi ya K-Mondo Sound imekamilisha video ya wimbo wake wa Magambo na tayari imekwishaanza kurushwa kwenye vituo mbalimbali vya video.
Kiongozi wa bendi hiyo, Richard Mangustino alisema jana mjini Dar es Salaam kwamba video hiyo imerekodiwa na kampuni ya NY Production iliyochini ya King Dodoo la Bouche.
“Tunashukuru kwamba video yetu imekamilika na imeanza kuonekana kwenye vituo mbalimbali vya televisheni na tunatarajia kuitambulisha rasmi kwa wapenzi wetu,” alisema.
Mangustino alisema baada ya kukamilisha video hiyo, wanatarajia kurekodi pia video ya wimbo wao mwingine uitwao Sharufa. Mangustino alisema baada hapo wanajipanga upya kwa ajili ya maonyesho yao ya kila wiki.
Alisema kwa sasa bendi yao inatumbuiza ijumaa pekee kwenye ukumbi wa Triz Motel, Mbezi Beach Dar es Salaam

Bunge la Namibia laitembelea benki ya wanawake Tanzania leo!

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto Mhe. Lucy Nkya akimpa vitabu mbalimbali kuhusu Maendeleo ya Jinsia na Wanawake kiongozi wa msafara wa wawakilishi wa Bunge la Namibia bw. Elia George Kayama
Mkuu wa Msafara wa wawakilishi wa Bunge la Namibia Mhe. Elia George Kayama akipata huduma za Kibenki katika Benki ya Wanawake

Wawakilishi wa Bunge la Namibia na Wajumbe a Kamati ya Maendeleo ya Jamii katika picha ya pamoja mara baada ya kutembelea benki hiyo.

LILIAN MDUDA ATINGA FAINALI ZA "FACE OF AFRICA" LAGOS NIGERIA!!

Meneja Masoko wa Multchoice Tanzania Furaha Samalu akizungumza na waandishi wa habari kweye Hoteli ya SouthernSun jijini Dar es salaam leo wakati akitoa taarifa juu ya mshiriki wa Mnet Face of Africa Lilian Mduda kutoka Tanzania kutinga katika fainali za shindano hilo zitakazofanyika nchini Nigeria katika jiji la Lagos Februari 6/ 2010 ambapo washiriki 10 kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika waliofanikiwa kuingia kwenye fainali hizo watachuana.
Tanzania ni moja ya nchi za Afrika ambazo zimekuwa zikipeleka wawakilishi mara kwa mara katika shindano hilo kubwa la uanamitindo katika bara la Afrika,
Kwa Tanzania mwanamitindo Miriam Odemba ndiye aliyewahi kushika nafasi za juu katika shindano hilo akiwakilisha Tanzania miaka ya nyuma na alifanikiwa kuingia mkataba wa kufanya kazi za uanamitindo na kampuni ya Elite Model Look ya Afrika Kusini.
Hata hivyo kampuni hiyo ilikatisha mkataba na Miriam Odemba na kumrejesha nyumbani baada ya mwanamitindo huyo kushindwa kufuata maelekezo ya kitaalamu aliyokuwa akipewa na wakuu wake katika kampuni hiyo ambapo inadaiwa alishindwa kufuata mpangilio mzuri wa kula chakula na mazoezi kitu kilichomfanya anenepe na kushindwa kukidhi viwango vya uanamitindo vilivyokuwa vikitakiwa na kampuni hiyo.
Mwakilishi wa mwaka huu Lilian Mduda ambaye ni mwanfunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam amesema amejiandaa vyema kwa ajili ya shindano hilo na haoni mshiriki yeyote anayemtisha isipokuwa ni yeye mwenyewe anayeweza kujiwekea mazingira ya kushinda kwa kuzingatia yale yote atakayoelekezwa na kuyafanya kwa ufanisi ili aweze kufikia malengo yake katika fainali hizo

Lilian Mduda mwakilishi wa Tanzania akiwa katika pozi.

Rais Kikwete afungua daraja la Mto Simiyu na Kuzindua mradi wa maji wilayani Meatu!!

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kuashiria kufungu rasmi daraja la Mto Simiyu,lililopo kati ya mpaka wa wilaya za Bariadi na Meatu,mkoa wa Shinyanga jana asubuhi
(picha na Freddy Maro)

Mbunge wa Bariadi Mashariki John Momose Cheyo(kulia), Mbunge wa Kisesa Mh.Luhaga Mpina (kushoto pembeni ya Rais) pamoja na viongozi wengine wa vyama vya siasa na serikali wakishangilia mara baada ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete kufungua rasmi daraja la mto Simiyu lililopo katika mpaka wa wilaya za Meatu na Bariadi mkoani Shinyanga jana mchana.Wanne kushoto ni Mama Salma Kikwete.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtwika maji Bi.Amina Ramadhani Mkazi wa kata ya Mwanuzi,wilayani Meatu, muda mfupi bada ya kuzindua mradi wa maji wa wilaya ya Meatu,mkoa wa Shinyanga.Kulia nia Waziri wa maji na umwagiliaji Profesa Mark Mwandosya na watatu kushoto ni Mama Salma Kikwete.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia mamia ya wakazi wa kata ya Mwandoya wilayani Bariadi jana mchana.

Tuesday, January 19, 2010

Wayahudi Waethiopia rukhsa Israel!!

Mmoja wa wanajeshi wa Israel ambaye ni myahudi methiopia.

Israel imeanza upya mpango wa kuwaruhusu wahamiaji wa Ethiopia wenye asili ya kiyahudi kuingia Israel baada ya kusitisha mpango huo kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Wahamiaji wapya 81 waliwasili na ndege iliyotoka Ethiopia kuelekea Tel Aviv siku ya Jumanne asubuhi.
Ndege hiyo ni ya kwanza kufika Israel tangu mwezi Agosti 2008, baada ya Israel kusema kuwa ina mpango wa kufunga mpango wa kuruhusu wahamiaji kuingia.
Jamii ya Falash Mura walibadili imani zao na kuwa wakristo baada ya kushinikizwa katika karne ya 19.
Baadhi yao takriban 8,000 ambao bado wako Ethiopia wanataka kuhamia Israel. WWW.BBCSWAHILI.COM

UN TANZANIA WREATH-LAYING CEREMONY IN DAR ES SALAAM!!

Today, Tuesday 19 Jan, 2010. UN staff in Tanzania joined other UN staff globally in the wreath-laying ceremony in honour of the victims of the earthquake in Haiti. The ceremony was held at the UN offices Compound in Kinondoni. Attached please find photos for your use.
( Photo; UN Tanzania/Mia B. Olsen)
UNDP Country Director, Mr Alain Noudehou, lays a wreath in front of the lowered UN flag in honour of the victims of the Haiti earthquake.
UN staff listening to the UNDP Country Director, Mr Alain Noudehou (not in the photo) when he was giving a message of solidarity in honour of the victims of the Haiti earthquake at a wreath-laying ceremony held at UN offices in Kinondoni, Dar es Salaam, on Tuesday, 19 Jan.


Mpinzani achaguliwa waziri mkuu Guinea!

Jean-Marie Dore.

Viongozi wa kijeshi wa Guinea wamemchagua kiongozi wa upinzani Jean-Marie Dore kuwa waziri mkuu, ikiwa ni hatua ya kurejesha utawala wa kiraia.
Msemaji wa jeshi hilo Idrissa Cherif amesema Bw Dore ana uzoefu na uelewa wa siasa za Guinea.
Bw Dore amekuwa mkosoaji mkubwa wa utawala wa kijeshi ambapo alilazwa hospitalini baada ya hatua ya wanajeshi kuzima maandamano tarehe 28 Septemba.
Jeshi lilishika madaraka Desemba 2008 lakini kiongozi wake Kapteni Moussa Dadis Camara alipigwa risasi na kujeruhiwa vibaya mwezi uliopita.
Kiongozi wa serikali ya mpito Jenerali Sekouba Konate anatarajiwa kurudi Conakry siku ya Jumanne, ambapo anatarajiwa kutangaza rasmi juu ya uteuzi wa Bw Doare

PLOTS FOR SALE AT KIGAMBONI_GEZAULOLE MWONGOZO FARM LOW DENSITY PLOTS NEAR THE BEACH!!


LOW DENSITY PLOTS AT BLOCK 4 PLOT NO.40 AND 38 each with square meters 1260.
The plots have Title Deeds and are almost half a kilometre from the beach Genuine buyers please contact below:

Tel: +255 713362901, +255754 362901

MAKANISA YATAKIWA KUWAJALI WANAKWAYA WAO ILI WAWEZE KUDUMU KATIKA KWAYA HIZO!!

Producer Frank Kameta akiwa ofisini kwake.

Producer wa siku nyingi ambaye ameshawatoa wasanii kibao wa muziki wa bongofleva anayejulikana kama Frank Kameta hivi sasa ameugeukia muziki wa injili baada ya kutamba katika muziki wa bongofleva kwa muda mrefu.
Akizungumza na Mwana FULLSHANGWE. BLOG Kameta amesema ameamua kuinga katika muziki wa injili kwakuwa huko hakuna Ubabaishaji wa kimuziki, kwa maana ya waimbaji wa muziki wa injili wanajua muziki mana yake nini na hakuna kazi kubwa ya kusahihisha makosa yao katika uimbaji kama vile waimbaji wa muziki wa Bongofleva lakini pia malipo yao ya kazi hayana matatizo sababu kazi zao zinatoka.
Producer huyo maarufu nchini anasema ni kazi kubwa kufanya kazi na wasanii wa bongofleva hasa wale ambao hawajui hata kupiga gitaa au kinanda (Keyboard) kwani hata kanuni za muziki hawajui hivyo mnapoingia studio atajitahidi sana atarekodi nyimbo nzuri kwenye albam ya kwanza lakini baada ya hapo anashindwa kuleta ubunifu mpya kwenye albam inayofuata hali inayomfanya apotee katika gemu ya muziki.
Kameta anasema tayari amesharekodi albam za waimbaji wa injili wengi na wenye majina makubwa na albam zao zinafanya vizuri sana katika soko.
Amewataja waimbaji hao kuwa ni Ambwene ambaye amerekodi albam ya Matatizo ni radha, Bahati Bukuku na albam yake Nimesamehewa dhambi siyo Majaribu, Neema Mushi albam Raha jipe mwenyewe, Bonny Mwiteje na wengine wengi.
Lakini pia anasema tayari ameshamaliza kurekodi albam ya Ramadhan Masanja (Banza Stone) inayoitwa Photo yenye nyimbo nane huku akizitaja baadhi ya nyimbo ambazo ni Photo yenyewe,Mama Africa,Siri yangu na nyingine nyingi.
Anasema kutokana na kubadili mwelekeo wake wa kazi anashukuru kwani ameweza kujua mambo mengi katika muziki na pia si haba riski inapatikana vizuri na watoto wanakwenda shule, lakini pia amewataka viongozi wa makanisa na waumini kubadili mwelekeo. wawajali wanakwaya wao na kuwalipa angalau posho kidogo kutokana na huduma yao ya uimbaji .
kwani kwa sasa muziki wa injili ni biashara nzuri ambayo inanufaisha makanisa tu wakati wanakwaya pia wanakabiliwa na matatizo mengi ya kimaisha na ndiyo, maana waimbaji wengi wamekuwa wakikimbia na kuanza kuimba kwa kujitegemea kitu ambacho kimeonyesha kuwapa ahueni, na kutokana na hilo wanakwaya wengi sasa hivi wanakimbia kwaya zao na kuanzisha vikundi vyao vya uimbaji kwa kumalizia akawasihi wakuu hao kuliangalia hili ili wawasaidie hawa wanakwaya lakini pia jambo hili litawafanya wanakwaya kudumu katika kwaya zao na kutoa huduma vizuri zaidi makanisani


WAZIRI BERNAD MEMBE AFUNGUA MKUTANO WA DIASPORA JIJINI DAR. LEO!!

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe akifungua mkutano wa wadau wa majadiliano baina ya wataalamu wa hapa nyumbani na wa nje jijini leo kuhusu uwezekano wa kuwashirikisha kikamilifu Watanzania walio nje ya nchi mkutano huo unaratibiwa na Wizara ya Nje ambayo tayari wameshaunda Idara ya DIASPORA.
(Picha na Mwanakombo Jumaa -MAELEZO).

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano Wakimataifa Bernard Membe (KUSHOTO) akiongea katika mkutano wa majadiliano baina ya wataalamu mbalimbali wa hapa nyumbani na wa nje jijini leo kuhusu uwezekano wa kuwashirikisha watanzania walioko nje kurudi na kuwekeza hapa nchini, Pichani mwingine ni Kiongozi wa shirika la kimataifa linaloshughulikia masula ya uhamiaji nchini (IOM- International Organizaion for Migration ) Mr.Par Liljert..
Baadhi ya wadau walioshiriki katika mkutano wa majadiliano ya wataalamu mbalimbali wa hapa na wa nje jijini leo wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe (hayupo Pichani ) wakati alipofungua mkutano wa majadiliano.

WASHINDI WA "FYATUA CHOO USHINDE" WAJIZOLEA ZAWADI!!

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Prof. David Mwakyusa akipata maelezo ya picha zilizoshinda katika kampeni ya Fyatua Choo Ushinde kutoka Mkurugenzi wa Afya na Mazingira Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bw. Elias Chinamo wakati wa maonyesho ya picha hizo na kuhitimisha kampeni hiyo iliyokuwa ikiendesha na Wizara hiyo, ambapo washindi kutoka mikoa mbalimbali walijishindia zawadi za simu, sabuni, ndoo , mabeseni pamoja na kujengewa vyoo vya kisasa, maadhimisho hayo yamefanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo.
Mshindi wa jumla wa Kampeni ya Fyatua choo ushinde iliyokuwa ikifanyika nchini kote Bi Fatma Ally kutoka mkoani Dodoma akipokea zawadi zake kutoka kwa mgeni rasmi Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Prof David Mwakyusa wakati wa kuhitimisha kampeni hiyo iliyofanyika kwenye viwanja vya mnazi mmoja leo Fatma kulia nia Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Aisha Kigoda.
Bendi ya Mjomba inayomilikiwa na mwanamuziki na mshairi maarufu hapa nchini Mrisho mpoto nayo ilikuwepo na kutoa ujumbe mbalimbali na burudani juu ya kuhamasisha wananchi kujenga vyoo bora ili kulinda afya zao na kujikinga na magonjwa ya miripuko.
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali nao wahuduria pia kama unavyowaona.

Mr. Mapunda kushoto akiwa na rafiki yake Joseph Ogutu katika maadhimisho hayo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja.
Sebo kutoka Magic Fm kushoto akiwa na wadau wengine waliohudhuria wakati wa kuhitimisha kampeni ya Fyatua Choo Ushinde iliyokuwa ikiendeshwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii na wadau mbalimbali wa Afya.

Miaka 30 ya huduma za Posta yaadhimishwa jijini Arusha!!

Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein akizindua mfumo wa anwani za nyumba na Mitaa Kitaifa katika eneo la Posta Kuu Mjini Arusha ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 30 ya huduma za Posta Barani Afrika. Kulia ni Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Profesa Peter Msola(Picha na Clarence Nanyaro… VPO).
Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein akionyeshwa kifaa ambacho kinaweka kumbukumbu za wshitiri wa anwani za nyumba na Mitaa na toka kwa muuzaji wa wakala wa kampuni ya ESCHER GROUP ya Ireland bwana Khalid Sadiki wakati wa maadhimisho ya miaka 30 ya huduma za Posta mjini Arusha.Wengine ni Waziri wa Mawasiliano Sayansi, naTeknolojia Profesa Peter Msola na Waziri wa Habari,Michezo na utamaduni George Mkuchika.

Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein akijadilia jambo na Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia,muda mfupi kabla Dk Shein hajafungua rasmi kongamano na maonesho ya huduma za Posta Barani Afrika kutimiza miaka 30 katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC)

President Kikwete meets Barrick's top management team in Mwanza!!

President Jakaya Mrisho Kikwete with Barrick's Gold Corporation top management team at Mwanza state Lodge yesterday evening.From left Barrick Tanzania Executive General Manager Mr.Deo Mwanyika, Aaron Regent Barrick's Chief Executive Officer and President of Barrick Gold Corporation(Second left), President Jakaya Kikwete, Kelvin Dushnisky Barrick Executive Vice President(fourth left) and Greg Hawkins Barrick's Chief Financial Officer(Photo By Freddy Maro)


Mkataba wa mifugo na uvuvi kati ya China na Tanzania

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi wa Tanzania John Magufuli ( kulia) akibadilishana hati na Waziri wa Kilimo wa China NIU DUN jijini jana katika sherehe ya kuwekeana saini mkataba wa makubaliano ya Mifugo na Uvuvi kati ya nchi za Tanzania na China . Picha na Mwanakombo Jumaa wa Maelezo.

Monday, January 18, 2010

KAMATI YA BUNGE YAJADILI MAENEO YA MABADILIKO KATIKA SHERIA MPYA YA MADINI

Waziri wa Nishati na madini Wiliam Ngeleja akiongea na wajumbe wa kamati Bunge ya Nishati na Madini (hawapo pichani)wakati wa mkutano wa siku mbili kujadili maeneo mbalimbali ya mabadiliko katika sheria ya madini ya mwaka 1998 na hatimaye kupata sheria mpya ya madini itakayotoa miongozo ya namna nchi itakavyofaidika kutokana na rasilimali hiyo leo wilayani Bagamoyo. PICHA NA ARON MSIGWA - MAELEZO.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kazi na kamati ya Bunge kujadili maeneo ya mabadiliko katika sheria ya madini ya mwaka 1998 na hatimaye kupata sheria mpya ya madini itakayotoa miongozo ya namna nchi itakavyofaidika kutokana na madini leo wilayani Bagamoyo.

Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Nishati na Madini wakiwa katika picha ya pamoja wakiongozwa na Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (katikati) mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa kazi na kamati ya Bunge kujadili maeneo mbalimbali ya mabadiliko katika sheria ya madini ya mwaka 1998 na hatimaye kupata sheria mpya ya madini leo wilayani Bagamoyo.


AKIL THE BRAIN A.K.A "REGINA" KUTOKA KIMATAIFA ZAIDI!

Akil The Brain katika pozi.

Msanii wa siku nyingi katika muziki wa kizazi kipya yaani Bongofleva anayejulikana kama Akil The Brain tayari yuko mbioni kutoa Albam yake ya pili itakayokuwa nyimbo za kiingereza tu ambyo ansema kwamba albam hiyo imelenga soko la nje zaidi tofauti na albam ya kwanza aliyotamba nayo sana ikiitwa (Regina).
Akil The Brain ameyasema hayo wakati akiongea na kamanda wa FULLSHANGWE katikati ya jiji la Dar es salaam ambapo amesema karibu nyimbo zote ziko tayari kwa ajili ya albam hiyo hivyo kilichobaki ni kukamilisha vitu vidogovidogo vilivyobaki ili ianze kutangazwa.
Amesema analenga soko lake zaidi nchini Uingereza ambako tayari kwa kuanzia ameshapata nafasi ya kufanya mahojiano na moja ya vituo vikubwa vya televisheni vya nchini humo ambacho kinajulikana kama MA TV na anatarajia kuafanya mahojiano hayo wakati wowote mwaka huu, ameongeza kwamba vituo vingine vya televisheni atakavyofanya navyo mahoniano ni ZEE CHANEL katika kipindi chake cha View Asia ambacho kinaonyesha wasanii mbalimbali chipukizi kutoka mataifa mbalimbali.
Akizungumzia nyimbo zilizomo katika Albami hiyo amesema ziko nyingi lakini akazitaja nyimbo kadhaa kama vile Whay, I am Alone, Suzana,Dont Daught my love, I am Moving, Your Mine,Pain is Healing na nyingine nyingi.
Akil The Brain anasema Albam yake ya kwanza imemtambulisha na kufanya afahamike katika nchi mbalimbali Duniani na anapata mialiko mingi sana hasa katika nchi za Asia na Ulaya na kwa sasa ameamua kuanzisha bendi ambayo inaundwa na wanamuziki watano ikiongozwa na yeye mwenyewe.
Amewataja wanamuziki wenzie katika bendi hiyo kuwa niyeye mwenyewe Akil, Big Jah Man,Zahil,Salim na Phantom bendi hiyo inafanya maonyesho katika Hoteli mbalimbali za kitalii jijini Dar es salaam na kufanya maonyesho katika maeneo mialiko mbalimbali na ukitaka kuwapata namba zao ni
0764777333/0754269218

FM ACADEMIA NA AFRICAN STARS HUKUNA MBABE KATIKA SOKA!!

kikosi cha timu ya Twanga Pepeta kikiwa katika picha ya pamoja katika mchezo wa vuta nikuvute uliofanyika jana kwenye viwabja vya Leaders Club ambapo timu hizo zikiwa zimesheheni wachezaji wake wengi wakiwa wanamuziki lakini pia vikichanganywa na Mamluki kidogo zilishindwa kutambiana katika mchezo huo uliokuwa ni wa kirafiki na kubadilishana mawazo kwa wanamuziki wa bendi hizo pamoja na mashabiki wake kwa ujumla, mpaka kipenga cha mwisho kinalia hakuna timu iliyoweza kuona lango la mwenzake na kufanya matokeo hayo kuwa 0-0.

Kikosi cha timu ya F.M Academia wazee wa Ngwasuma nacho kikiwa katika picha ya pamoja.

National Officer (NOB) Communication for Development (1 Year Only)

UNICEF is seeking an energetic, creative communication professional to
support programmes for children in Zanzibar. The successful candidate will
help develop and implement behaviour change communication strategies for
child survival, to protect children from violence, and to encourage children to
stay in school. He/She will also play a key role in supporting advocacy for
children’s issues with the government, media, civil society and the public.
If you are the right candidate for this post you are a dedicated, articulate,
communication professional, with at least two years experience working in
social communication. You have a degree in communication, social science
or related field, and have a natural flair for working in teams. You are fluent in
both English and Kiswahili, and have strong writing abilities. You understand
some of the challenges involved in behaviour change communication and
you may have some experience in radio and/or visual communication.
If you are interested in this special one year assignment in communication for
development with UNICEF in Zanzibar please send your CV and a letter of
application outlining your relevant experience and explaining why you are
best suited for this position.
Your application letter and CV should be sent to hr.tanzania@unicef.org by
Monday 1 February 2010.
UNICEF is an equal opportunity employer. Women are encouraged to apply.
Only short-listed candidates will receive a response..

NEW HABARI 2006 LTD WALA MNUSO WA KUUKARIBISHA MWAKA 2010!!

Mwandishi Said Makala aka (ndugu yake na hela) kulia akigonganisha galasi na Baadhi ya Wafanyakazi wa New Habari 2006 Ltd, wakati wa sherehe yao ya kuuaga mwaka 2009 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2010, iliyofanyika jana usiku kwenye Hoteli ya Giraffe Ocean View, iliyopo Mbezi beach Dar es Salaam, wadau wa FULLSHANGWE wanawatakia kila mafanikio katika mwaka huu mpya wa 2010 katika mipango na kazi zenu za kuupasha habari umma wa Watazania

Mwandishi wa habari mwandamizi wa gazeti la The African linalochapishwa na kampuni ya New Habari 2006 Ltd Siddy Mgumia akiongoza pamoja na Mwani wakiongoza wenzao katika kucheza Miondoko ya Mduara, kwenye Sherehe Hiyo ya kuaga mwaka na kuukaribisha mwaka mpya 2010.

Ni Sebene tuuuu kwa kwenda mbele, ilikuwa ni furaha ya kumaliza mwaka 2009 na kuuanza mwaka mpya wa 2010 bila matatizo katika majukumu ya kazi.

Mhariri wa Habari wa gazeti la Rai, Mayage S. Mayage (kulia) akiwa katika pozi na baadhi ya wafanyakazi wenzake wakati wa sherehe hiyo

Herieth Mandari (kushoto) na Rachel Mwiligwa, wakila pozi katika meza yao isiyosheheni kilaji eti hawatumii kilaji sijui ni kweli???????? ama zuga tuuuuuu!...., wakati wa Sherehe ya wafanyakazi wa New Habari (2006) Ltd, ya kumaliza mwaka 2009 na kuukaribisha mwaka 2010, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Ocean View Giraffe Mbezi Beach Dar es Salaam juzi usiku.

Mapigano mapya Jos, Nigeria

Moja ya picha ikionyesha vurugu za mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyowahi kutokea nchini Nigeria.

Ripoti kutoka nchini Nigeria zinasema kuwa mapigano makali yamezuka katika mji wa Jos, kati kati mwa nchi hiyo.
Watu saba wameripotiwa kufa na wengine wengi kujeruhiwa.
Mamia ya familia yametoroka makazi yao na sasa wanalala katika kambi za muda.
Mapigano hayo yalitokea katika wilaya ya Nassarawa Gwom, magharibi mwa mji wa Jos.
Mfanyakazi mmoja wa shirika la kutoa misaada ambaye alizungumza na BBC, amesema kuwa takriban watu 58 wamepelekwa hospitalini kwa matibabu, wengi wakiugua majeraha ya kukatwa katwa na panga.
Polisi wa kutuliza ghasia na wanajeshi wa Nigeria wanashika doria katika mitaa ya mji huo na wameweka agizo la kutotoka nje usiku kucha.

Sunday, January 17, 2010

SIMBA MWENYE KIU AVAMIA KISIMA CHA MAJIMAJI!!

Kikosi cha timu ya Simba.

Timu ya Simba ya jijini Dar es salaam leo imeibanjua timu ya Majimaji kutoka Somgea Mkoani Ruvuma magoli 2 kwa Nunge katika mchezo mkali na uliokuwa wa upande mmoja uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru maarufu kama shamba la bibi.
Katika mchezo huo timu ya Simba ndiyo iliyotwala sana mchezo huku wachezaji wake wakikaa na mpira kwa muda mrefu na kufanya mashambulizi ya mara kwamara kwenye lango la timu ya Majimaji, amabpo magoli ya simba yamefungwa na mshambuliaji wake hatari Mussa Hassan Mgosi aliyefunga katika dakika ya 37 kipindi cha kwanza na 72 katika kipindi cha pili hivyo kuifa simba kuibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya majimaji.
Majimaji walifanya mashabulizi machache katika lango la timu ya Simba ambayo hayakuwa na madhara yoyote langoni mwa Simba hivyo kuwafanya wekundu hao wa msimbazi kuusogelea zaidi ubingwa wa Ligi kuu ya Vodacom 2010 ambao kwa sasa unashikiliwa na timu ya Yanga ya Jijini Dar es salaam.
Simba yenye pointi 36 baada ya ushindi mnono wa leo inahitaji kushinda michezo minne ili iweze kutangaza ubingwa kwa msimu huu wa 2010-2011 kazi ambayo kocha mkuu wa timu hiyo mzambia Patrick Phiri amesema atahakikisha anashinda michezo hiyo ili aweze kutangaza ubingwa mapema zaidi

Mwanamuziki Huseni jumbe atua Msondo!!

Waimbaji wa bendi ya Msondo music wakiwajibika wakati wa onesho lao lililofanyika Dar es salaam jana Kushoto ni Juma Katundu na Huseni Jumbe.(Picha na msondo)

Na Mwandishi Wetu
BENDI kongwe ya muziki wa Dansi nchini ya Msondo Music imemrudisha kundini mwimbaji wake mahili, Huseni Jumbe 'Mzee wa Dodo' baada ya kukaa nje ya bendi hiyo kwa mwaka mzima
Akizungumza Dar es Salaam jana, Msemaji wa bendi hiyo, Rajabu Mhamila 'Super D'Alisema, wameamua kumrudisha kundini mwimbaji huyo baada ya kukaa na viongozi na kukubaliana nae mambo kadhaa, hivi sasa ameshaanza kupanda katika jukwaa la bendi hiyo ambapo tunajipanga kutoa nyimbo mpya za mwaka huu baada ya mwaka jana kutambulisha albamu yetu ya "Huna shukrani" ambayo iko mtaani kwa sasa ikiuzwa katika maduka mbalimbali ya muziki
Wakati huohuo, bendi hiyo kwa sasa imekuwa ikitoa burudani za wazi katika kuwaweka karibu wapenzi wake ambapo kila jumamosi inakuwa katika viwanja vya TCC Chan'gombe na jumapili inakuwa Leaders Club Kinondoni jijini Dar es Salaam
Alisema, sambamba na burudani hizo pia wamejipanga kutoa nyimbo mpya kila baada ya wiki tatu ili kukamilisha albamu ya mwaka huu mapema kadiri iwezekanavyo alisema Mhamila, huku
Akitoa wito kwa wapenzi wa bendi hiyo kuhudhuria maonesho yao popote yafanyikapo kwani kuna burudani ambazo hazihitaji kuhadithiwa

Saturday, January 16, 2010

YANGA WAIKUNG"UTA AFRICA LYON KWEUPEE!!

Mshambuliaji wa Yanga Mrisho Ngasa akiwatoka mabeki wa timu ya Africa Lyon katika mchezo wao uliofanyika uwanja wa Uhuru leo.

Mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom umeanza leo kwa kuzikutanisha timu za Yanga ya Dar es salaam ambao ni mabingwa watetezi wa ligi hiyo na Africa Lyon zamani Mbagala Market zilizopepetana kwenyu uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam
Katika mpambano huo wa kufungua ligi katika mzunguko wapili timu ya Yanga imeibuka mshindi baada ya kuikandamiza timu ya Africa Ryon iliyoonyesha mchezo wa kusuasusa kutokana na kucheza mpira katika kiwango cha chini hivyo kuwafana wapoteze mipira mara kwa mara walipoingia kwenye lango la timu ya Yanga.
Yanga imeanza vyema ligi hiyo baada ya mchezaji wake Jerry Tegete kutumbukiza mpia katika lango la Africa Lyon huku mabeki wa timu hiyo wakijaribu kuokoa bila mafanikio, katika kipindi cha pili yanga iliweza kuongeza goli lingine kupitia kwa mshambuliaji wake machachari Mrisha Ngasa hivyo kuyafanya matokeo hayo kuwa Yanga 2 na Africa Lyon 0.

NANI MKALI KATIKA SOKA FM ACADEMIA NA AFRICAN STARS (TWANGA PEPETA)

Wanamuziki wa bendi za African Stars na Fm Academia wanatarajia kupepetana katika mchezo wa mpira wa miguu januari 17/2010 katika bonanza linalofanyika kila jumapili kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam.
Meneja wa bendi ya Fm Academia aliyefahamika kwa jini moja Mujibu amesema mchezo huo utafanyika kuanzia saa nane mchana kwa bendi hizo kucheza mpira wa miguu pambano ambalo litakuwa ni la kirafiki
Mujibu ameongeza kuwa lengo la mpambano huo ni kuwakutanisha wanamuziki wa bendi zote mbili lakini pia ni kujenga mahusiano mema kati ya wanamuziki wetu kwa kuwa muziki ni burudani na kila mtu anatakiwa kufurahia kazi yake ya muziki lakini pia ni wakati mzuri kwa wanamuziki wetu kubadilishana mawazo na mbinu za kimuziki.
Kama unavyoona katika picha hapa ni wanamuziki wa African Stars na FM Academia wakifanya mazoezi kwa pamoja kwenye viwanja hivyo vya Leaders kabla ya mchezo huo wa kesho wadau kaeni mkao wa kupashwa kwani mara baada ya mpambano huo kesho tutakuletea matokeo yake na mtajua nani ameibuka mshindi.

TAARIFA YA MSIBA WA MACHALO MAJIGE FAUSTIN, AU (SAMSON MUKANDYA)


Familia ya Marehemu, Bw & Bibi, Aloycius Chokara, wa Sinza Mori Dar-es-salaam.

Inasikitika kutangaza kifo cha Mtoto wao mpendwa MACHALO MAJIGE FAUSTIN, AU (SAMSON MUKANDYA) kilichotokea tarehe 14, 01, 2010, katika hospitali ya Muhimbili Dar-es-salaam, msiba upo nyumbani kwao Sinza Mori, Mazishi yatafanyika Tarehe 16, 01, 2010, katika makaburi ya Sinza. Saa sita kamili kutakuwa na ibada katika Kanisa Katoliki la (Mt Maxcimilian Kolbe Mwenge)Baada ya ibada, mwili wa marehemu utapelekwa nyumbani kwao Sinza mori.Saa nane kamili, ndugu jamaa na marafiki watatoa heshima za mwisho kwa marehemu, na baada ya heshima za mwisho, safari ya kuelekea makaburini itaanza. Watu wote mnaomfahamu MACHALO, karibuni sana ili tumsindikizendugu yetu na rafiki yetu, katika safari yake ya mwisho hapa duniani.Kwa taarifa zaidi unaweza kupiga simu namba hizi, 0713652020, Joseph, 0713472930, Mang´enya, 0713131910, Samora. Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe, apumzike kwa amani amen.

Friday, January 15, 2010

YAHYA ISSA NA CASTOR MUMBALA WAPASUA VICHWA VYA WAKUU WA AFRICA LYON FC!!

Uongozi wa timu ya Africa Lyon ya jijini Dar es salaam umesema uko katika kikao kizito jioni hii na shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF ili kumaliza tatizo la wachezaji wa timu hiyo Castor Mumbala na Yahya Issa waliokuwa wameachwa na timu hiyo katika dirisha dogo la usajiri uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana.
Afisa habari wa timu hiyo Kambi Mbwana amesema mpaka jioni hii viongozi wa timu hiyo na TFF wako kwenye kikao cha kujadili suala hilo na watamalizana na wachezaji hao jioni hii ili waendelee kulipwa mshahara wao na timu hiyo mpaka mkataba wao utakapomalizika.
TFF ilikuwa imewazuia wachezaji watatu wapya waliosajiriwa na Africa Lyon kucheza kwenye mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom ambao ni golikipa Ivo Mapunda kutoka Saint George ya Ethiopia, Meshack Abel na Adam Kingwande kutoka klabu ya simba ya jijini Dar es salaam, kutokana na mkanganyiko wa taratibu za usajiri uliojitokeza kwa wachezaji Castor Mumbala na Yahya Issa.
Kambi amesema timu hiyo imeamua kuwarejesha kundini wachezaji hao ili kuiwezesha timu hiyo kufanya vyema katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ambapo timu hiyo inatarajia kucheza na mabingwa watetezi wa ligi hiyo timu ya Yanga, mchezo utakaochezwa jumapili kwenye uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam, Africa Lyon inatarajia kwatumia wachezaji wake wapya ili kuimarisha kikosi chake na kukiwezesha kuanza vizuri ligi hiyo katika mzunguko wa pili na wa lala salama.

Twanga Pepeta 'Kupigisha Simu' Kiwalani januari 29 ijumaa!!


BENDI ya muziki wa dansi ya African Stars 'Twanga Pepeta International' inatarajia kuwapa mashabiki wake wa Kiwalani, Dar es Salaam, burudani ya staili yake mpya iliyoshika kasi ya 'Kupigisha Simu' kwenye ukumbi wa Koyanga Night Park.
Mkurugenzi wa Kampuni ya First Entertainment iliyoandaa onyesho hilo, Victorian Nachenga 'Victor Buguruni', alisema Dar es Salaam jana kuwa bendi hiyo itafanya onyesho hilo Ijumaa (Junuari 29, mwaka huu) kuanzia saa 3 usiku kwa kiingilio cha sh. 5,000.
Victorian alisema Twanga Pepeta pia itawapa mashabiki wao staili ya 'Sugua Kisigino' katika onyesho ambalo pia ni sehemu ya kuendelea kukaribisha mwaka mpya 2010 na 'kurudi nyumbani' kwenye ukumbi huo uliopo Kiwalani Kijiwe Samli.
Mkurugenzi huyo alisema onyesho hilo pia litapambwa na burudani kutoka kwa wasanii wengine watakaotangazwa baadaye.
Twanga Pepeta inayotamba na albamu ya 10 ya bendi hiyo, Mwana Dar es Salaam, itapiga nyimbo zake saba mpya zikiwamo Sumu ya Mapenzi uliotungwa na Khalid Chuma 'Chokoraa', Ubaya Aibu (Saulo John 'Ferguson'), Sitaki Tena (Saleh Kupaza), Nazi Haivunji Jiwe (Thabit Abdul).
Nyingine ni Rafiki Adui uliotungwa na Rogart Hega 'Katapila' na Shida Darasa na Mwana Dar es Salaam uliobeba jina la albamu, zilizotungwa na Charles Gabriel 'Chaz Baba'.
Albamu nyingine ambazo Twanga Pepeta imewahi kutoa na kutamba katika anga za muziki nchini ni Kisa cha Mpemba mwaka 1999, Jirani (2000), Fainali uzeeni (2001), Chuki binafsi (2002), Ukubwa jiwe (2003), Mtu pesa (2004), Safari 2005 (2005), Password (2006) na Mtaa wa Kwanza (2007).

Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameiomba Serikali ya China kusaidia Sekta ya kilimo!!

Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda.
Benjamin Sawe
Maelezo Dar es Salaam
Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameiomba Serikali ya China kuendelea kuwa na ushirikiano na Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na sekta ya kilimo.
Akiongea na Waziri wa Biashara na Masoko wa China bwana Chen Deming Waziri Pinda alisema sekta ya kilimo nchini imekuwa haifanyi vizuri kwa miaka mingi licha ya kuwa asilimia kubwa ya Watanzania kutegemea kilimo.
Licha ya kuwekeza kwenye kilimo Waziri Pinda aliwaomba kulifufua Shirika la Tazara kwani reli hiyo kwa miaka ya nyuma imekuwa ikichangia kwa kiasi kikuba katika uchumi wa Taifa.
Aidha Waziri Pinda alisema reli ya Tazara imekuwa tegemeo kubwa la nchi za jirani kwani imekuwa ikisafirisha mizigo mbalimbali hivyo kuliingizia pato taifa.
Nae Waziri wa Viwanda na Masoko wa China Waziri Chen Deming alisema Serikali ya China itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika sekta mbalimbali ili kudumisha ushirikiano.
Waziri Deming alisema China itatuma wataalamu mbalimbali ikiwa ni pamoja na wakandarasi wa reli ili kuangalia uwezekano wa kuifanyia ukarabati njia ya reli ya Tazara.
Serikali ya Tanzania na China zimekuwa zikishirikiana kwa muda mrefu katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na kilimo,ujenzi wa uwanja wa Taifa wa Michezo,elimu na ujenzi wa shirika la Tazara.

Tamasha la wapenzi wa jinsia moja kuandaliwa Uchina!

Uchina inaandaa tamasha la kwanza kwa wapenzi wa jinsia moja baadaye leo katika mji Mkuu wa Beijing.
Wanaume wanane watawania taji la Mume Mrembo zaidi miongoni mwa wanaume wenye jinsia moja nchini humo.
Tamashi hiyo ni ishara ya uwazi nchini Uchina kuhusiana na wapenzi wa jinsia moja.
Hali hiyo ilikuwa haramu nchini humo hadi mwaka wa 1997 wakati hali hiyo ilifahamika kama ugonjwa wa kiakili hadi miaka tisa iliyopita.

WHO YATOA MAGARI 25 KUBORESHA AFYA YA MAMA NA MTOTO NCHINI!!

Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Bw. Martins Ovberedjo akimkabidhi nyaraka mbalimbali za magari yaliyotolewa leo na Shirika la Afya Duniani kusaidia mpango wa Afya ya mama na mtoto na pia juhudi za kupunguza vifo vya watoto walio chini ya umri wa miaka 5 nchini.(Picha na Aron Msigwa - MAELEZO).

Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Bw. Martins Ovberedjo akimkabidhi ufunguo wa gari Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Aisha Kigoda leo jijini Dar es salaam. WHO imetoa magari 25 kusaidia mpango wa kuboresha afya ya mama na mtoto na pia kupunguza vifo vya wanawake na watoto walio chini ya umri wa miaka mitano nchini.



KAMATI YA KUDUMU YA MAENDELEO YA JAMII YATEMBELEA TaSUBa - BAGAMOYO!

Naibu waziri wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Joel Bendera akifafanua jambo kwa kamati ya kudumu ya Bunge ya maendeleo ya Jamii kuhusu mpango wa serikali wa kuiboresha Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) mara baada ya kamati hiyo kukagua maeneo mbalimbali. (Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
Mbunge wa Mbinga Magharibi Capt. John Komba ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii akichangia mjadala kuhusu hali ya utamaduni nchini wakati wa majumuisho ya ziara ya kamati hiyo katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo jana mchana.

Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Bw. Juma Bakari akitoa ufafanuzi kwa kamati ya kudumu ya Bunge ya maendeleo ya Jamii mara baada ya kuwasili jana mchana kuhusu mkakati unaoendelea wa kuiboresha Taasisi hiyo katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya elimu na Miundombinu. Kushoto ni mwenyekiti wa kamati hiyo Mh. Jenista Muhagama na Naibu waziri wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Joel Bendera.



Maureen Lupo Lilanda Sauti za Busara Festival Artists 2010!!


Style
band, pop, traditional, urban
Festivals
Sauti za Busara 2010
Website
www.myspace.com/maureenzammo
Recordings
Evolution, 2002Tetwe, 2005Soul Masala, 2007
Feb 2010
Fri 12, 6:00pm Old Fort - Mambo Club
Maureen Lupo Lilanda aka “Mama Zambia” or fondly known in Zambia as “Aunty Maureen” is a singer-songwriter from Zambia. Endurance, patience and generosity characterise Maureen best. For the past twenty years she has travelled extensively both locally and internationally consistently grabbing the attention of listeners and fans. Broadening her musical genres from a subdued cabaret-jazz singer to an African vocalist, Maureen blends modern beats and rhythms with authentic sounds from Zambia. A four time recipient of the National Arts Council Award for Best Female Artist, she continues to give her time and experience to musical peers. She spent time as leader of the accapella group Amashiwi and during her long and illustrious career has shared stage with Black Voices (UK), Oliver Mtukudzi (Zimbabwe), Magic System (Cote d'Ivoire) and Baaba Maal (Senegal).

Thursday, January 14, 2010

Rais Kikwete ahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Guebuza Msumbiji!!

Rais Armando Emilio Guebuza wa Msumbiji akinyoosha juu katiba ya Msumbiji muda mfupi baada ya kula kiapo kuendelea kuingoza nchi hiyo kwa muhula wa pili wa Urais katika sherehe zilizofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo Maputo.Kushoto ni Rais wa Mahakama ya katiba wa Msumbiji Luis Mondlane aliyemwapisha Rais Guebuza.(picha na Freddy Maro)

Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini akiteta jambo na Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa sherere za kuapishwa kwa Rais Armando Emilio Guebuza kendelea kuingoza Msumbiji katika muhula wa pili wa Urais jijini Maputo.Katikati ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete




Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini akisisitiza jambo wakati akizungumza na Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wao Rais Armando Emilio Guebuza wa Msumbiji katika ikulu ya Mjini Maputo muda mfupi baada ya Rais Guebuza kuapishwa kuendelea kuingoza nchi hiyo katika muhula wa pili wa urais.





FIFII MOTO KUWAKAMATA WAPENZI WA TAARAB JANUARI 24, TRAVELTINE!!

Maimartha wa Jesse akiongea na wanahabari jijini Dar es salaam leo wakati alipotangaza onyesho kabambe la miondoko ya Taarab linalotarajiwa kufanyika januari 24 kwenye ukumbi wa Traveltine ambalo litajulikana kama Paty Kali la Kufungua mwaka 2010.
Maimartha amesema onyesho hilo litawahusisha wakali wa muziki wa taarab Afrika Mashariki ambo ni Jahazi Molden Taarab, malkia wa mipashi nchini Khadija Kopa na mkali wa kunengua kutoka Nairobi nchini Kenya Fifii Moto ambaye tayari yuko jijini kwa maadalizi kadhaa ya mtikisiko huo wa miondoko ya Taarab.
Maimartha ambaye ni afisa uhusiano wa onyesho hilo amewakaribisha wapenzi wa taarab jijini kuwa tayari kwa burudani nzuri itakayoletwa na wanamuziki hao wakali katika muziki huo akiongezea kuwa Fifii Moto amekuja kuwashika wapenzi na mashabiki wa taarab kwa kiuno chake.
Fifii Moto akionyesha jinsi ya kukata mauno juu ya meza mara baada ya kuzungumza na wanahabari jijini leo.


RAIS JAKAYA AKUBALI KUONGOZA KAMPENI YA "MARALIA HAIKUBALIKI TUSHIRIKIANE KUITOKOMEZA"

Aliyekuwa Balozi wa Marekani nchini Mark Green akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari kwenye Hoteli ya Movenpick wakati wa uzinduzi wa kampeni ya "Malaria Haikubaliki: Tushirikiane Kuitokomeza"
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Prof. David Mwakyusa katikati akisikiliza jambo wakati aliyerkuwa Balozi Marekani nchini Mark Green alipokuwa akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni ya kutokomeza Maralia kwenye Hoteli ya Movenpick leo, kulia ni Peter Peter Chernin (Mwenekiti wa Malaria no More Marekani ) ambaye ameungana na Balozi Mark Green katika kampeni hiyo na kulia ni Naibu waziri wa Afya Aisha Kigoda.

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imetangaza kuwa leo mheshimiwa Raisi Jakaya M. Kikwete amekubali kuongoza kampeni ya Malaria Haikubaliki: Tushirikiane Kuitokomeza .Leo Wizara imeungana na wasanii mashuhuri wa Tanzania, washirika wa kimataifa na viongozi wa serikali, wafanyabiashara na vitengo vya sanaa kulitangazia Taifa tamasha la zinduka hapo tarehe 13 februari katika viwanja vya leaders club jijini Dar es salaam. Tamasha hili ni kwajili ya kuwahamasisha watanzania katika kupambana na malaria.
Mwaka huu, Tanzania itakuwa nchi ya kwanza barani Afrika kufanikisha zoezi la utumiaji wa chandarua ya mbu na kutolewa kwa gharama nafuu kwa raia wake. Katika kuhamasisha juhudi hizi, Raisi kikwete na Malaria haikubaliki inahamasisha kila mtanzania kuwa na jukumu la kujilinda mwenyewe na familia yake katika kuidhibiti malaria.
Tanzania, kama kiongozi wa kupambana na malaria ulimwenguni, inahamasisha sekta zote za kijamii zikiwamo sekta za sanaa, biashara, na michezo kujumuika pamoja kupambana na malaria nchi nzima.
Chini ya uongozi wa Raisi na wizara ya afya na ustawi wa jamii kampeni hii ya uhamasishaji imelenga kila jamii ya kitanzania ili kubadili mtazamo wa watanzania juu gonjwa hili la malaria. Matokeo ya juhudi hizi ni kuongeza ujuzi zaidi wa kujikinga na malaria kama kulala ndani ya chandarua kilichowekwa dawa, tambua na itibu malaria mapema na hakikisha unajali na kuangalia afya ya mama mjamzito.
“Waafrika wengi hudhani malaria haiepukiki, na kwamba hakuna wanachoweza kufanya katika kuzuia gonjwa hili. Tunakwenda kuwahakikishia kuwa sio sahihi. Tunaweza kupunguza vifo vitokanavyo na malaria” alisema Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii David Mwakyusa “pamoja na mheshimiwa Raisi Jakaya M. Kikwete ninaamini kila Mtanzania atajiunga pamoja kutamka kuwa malaria haikubaliki nchini kwetu 2010.
Katika shughuli za mwaka 2010, Raisi Kikwete ataongoza tamasha la kitaifa liitwalo zinduka litakalowashirikisha wasanii mashuhuri wa Tanzania akiwamo msemaji mkuu wa tamasha hili lady Jay dee, Professor Jay, Tanzania House of Talent (THT na wengine wengi. kupitia vituo vya luninga na redio ujumbe wa tamasha hili utaweza kuwafikia mamilioni ya watanzani na ujumbe mahususi wa kutambua jukumu lao katika kujikinga na ugonjwa wa malaria. kwa kuongezea wasanii mahiri wa Tanzania wametunga wimbo unaozungumzia athari za ugonjwa wa malaria, wimbo uliowashirikisha wasanii 18, ushirikino mkubwa wa wasanii ambao haujawahi kufanywa hapa Tanzania.Wimbo huo umetambulishwa kwa waandishi wa habari na utaimbwa siku ya tamasha la zinduka
Ulimwengu wa muziki unanafasi kubwa katika kufikisha ujumbe kwa watanzania katika kupambana na malaria na kupata mafanikio makubwa katika kupambana na ugonjwa huu, alisema lady jay dee kama msemaji wa kampeni hii “katika tamasha la zinduka watanzania wote wataweza kupaza sauti zao kwa njia ya wimbo kwa nia moja ya kusitisha malaria nchini.
katika kuisaidia tanzania kupambana na malaria Malaria Haikubaliki itajumuisha shughuli za ushirikiano za kijamii, PSAs, ujumbe kwa njia ya luninga na radio,mabango,ngazi ya jamii,kiutamaduni, matukio ya kimichezo na maonyesho ya barabarani ili kuhakikisha ujumbe wa malaria haikubaliki unaufikia kila familia nchini Tanzania. kampeni hii ya kitaifa itakuwa kwenye engo zote za ngazi ya kijamii na kila nyumba kwa kuhamasisha shughuli za kijamii zitakazotolewa na Population Services International ,Johns Hopkins University na shughuli za district advocacy zitakazoongozwa kwa sauti moja.kwa wakati huo chama cha msalaba mwekundu Tanzania kitakuwa pamoja na katika kampeni za nchi nzima
Kutoka kwenye jamii ya imani Malaria Haikubaliki imehusisha baraza la kiristo nchini na baraza la kiislam kuwahusisha viongozi wa kiimani na waumini wao kuweka juhudi katika kupambana na malaria nchi nzima
Barani Africa malaria haiathiri maisha ya watu tu bali jamii nzima, malaria inasababisha mtu mmoja kukosa kazini kwa siku kumi na tano ndani ya mwaka na familia inatumia zaidi asilimia 25 ya kipato cha familia katika kutibu malaria barani Africa. Malaria ni kikwazo katika maendeleo, inakadiriwa barani Afrika dola bilioni 12 kila mwaka zinapotea na asilimia 40 zinatumika katika masuala ya afya.katika kupambana na ugonjwa huu, Tanzania imeweza kuonyesha jinsi Africa peke yake inavyoweza kujikwamua kutoka kwenye mzigo wa malaria na kuendeleza mikakati yake ndani na nje ya mipaka.
Malaria Haikubaliki: Tushirikiane Kuitokomeza inaongozwa na serikali ya Tanzania na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. Washirika wengine katika kampeni hii ya kupinga malaria ni Roll Back Malaria Partnership, Malaria No More, Population Services International, Johns Hopkins University Center for Communication Programs, Tanzanian Red Cross, United Against Malaria, MEDA na World Vision with support from the Global Fund.

Camara afanya mazungumzo ya dharura!!

Rais wa Burkina Faso amefanya mkutano wa dharura na kiongozi wa kijeshi wa Guinea aliyejeruhiwa Kapteni Moussa Dadis Camara na naibu wake Sekouba Konate.
Mazungumzo hayo yaliyofanywa kwa siri yalihusu khatima ya Kapteni Camara kufuatia kushindwa kwa jaribio la kumwuua mwezi uliopita.
Aliwasili Burkina Faso siku ya Jumanne akitokea Morocco, alipokuwa akipata matibabu ya jeraha alilolipata kutokana na kupigwa risasi.
Upinzani umesema unataka Kapteni Camara asijihusishe kwenye siasa kwa muda.
Jenerali Konate, ambaye amekuwa akishikilia madaraka kwa kipindi cha wiki sita tangu Kapteni Camara akipata matibabu huko Rabat, ameshaanza mazungumzo na upinzani.
www.bbcswahili.com

MCHEZAJI MORO UNITED AYEYUKA


Mrisho Ngasa mchezaji wa timu ya Yanga akimiliki mpira mbele ya beki wa timu ya moro United Oscar Joshua huku Jerry Tegete akianagalia katika moja ya mchezo uliochezwa katika mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom.

WAKATI timu za Ligi Kuu zikiwa katika maandalizi mazito ya kuuanza mzunguko wa pili wa ligi hiyo kuanzia mwishoni mwa wiki hii, uongozi wa timu ya soka ya Moro United, unamsaka beki wake aliyesajiliwa hivi karibuni katika dirisha dogo la usajili, Abdallah Matanda.
Kwa mujibu wa Msemaji wa Moro United, Eric Anthony, Matanda aliyewahi kuichezea Prisons ya Mbeya, hajaonekana mazoezini, licha ya hivi karibuni kuchukua vifaa vya timu kwa ajili ya mazoezi.
“Ni kweli, tunamtafuta kwa sababu hatujui kilichomsibu. Tangu achukue vifaa vya mazoezi hajaonekana na hata kocha, Juma Mwambusi na wasaidizi wake hawana taarifa. Mbaya zaidi ni kwamba hapatikani kupitia simu yake ya mkononi,” alisema Anthony na kuongeza kwamba; “Tunamuomba aripoti kambini haraka au popote alipo awasiliana na uongozi.”
Ukiachana na Matanda, msemaji huyo ameelezea kufurahishwa na maandalizi ya timu yake, akidai inaonyesha matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika mzunguko wa pili.
Moro inayoshika nafasi ya tisa kati ya timu 12 kutokana na kuwa na pointi tisa, itaanza mzunguko wa pili Januari 19 kwa kucheza na Toto African ya Mwanza kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Kwa sasa timu hiyo inajifua asubuhi na jioni kwenye viwanja vya Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

SERENGETI YAKANUSHA HABARI ZILIZOANDIKWA KWENYE GAZETI LA NEW VISION (UGANDA)

Katibu mkuu wa shirikisho la mpira Tanzania TFF Fredrick Mwakalebela akizungumza na wanahabari kwenye makao makuu ya kiwanda cha bia cha Serengeti Chang'ombe Temeke jijini Dar es salaam, anayefuatia katika picha ni Meneja uhusiano wa kamuni hiyo Teddy Mapunda na mwisho ni Msemaji wa TFF Frolian Kaijage.
Gazeti la New Vision la Uganda toleo la Januari 6/ 2010 lilichapisha habari likieleza kuwa Kampuni ya Bia ya Serengeti ndiyo iliyokataa maombi ya Uganda ya kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki na timu ya Taifa ya Ivory Coast wakati timu hiyo ilipokuwa Tanzania kujiandaa na fainali za mataifa ya Afrika zinazoendelea huko nchini Angola. Gazeti hilo liliendelea kudai kuwa uamuzi wa Ivory Coast kucheza na Rwanda ulikuwa baadaye kwani Serengeti ilitaka Ivory Coast icheze michezo miwili na Taifa Stars kwa madai kuwa Serengeti ilitaka kurejesha fedha ambazo ziliwekezwa kwenye ziara hiyo.
Habari hiyo ambayo kwa hakika haina ukweli wa aina yoyote ilimnukuu afisa wa Shirikisho la mpira wa miguu la Uganda FUFA aitwaye Moses Magogo akitoa madai hayo. Hata hiyo habari haikueleza Magogo ana cheo gani ndani ya FUFA.Serengeti Breweries inapenda kuufahamisha umma kuwa majukumu yake katika mpira yanafahamika vizuri kulingana na Mkataba ambao inao na Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF.

Kazi ya SBL ni kutoa fedha kwa ajili ya kulipia gharama kama zilivyoainishwa kimkataba.Si kazi ya SBL kualika timu za kucheza wala kuamua ni timu gani icheze na Taifa Stars au timu nyingie yoyote ile. Hiyo ni kazi ya TFF.Kwa mantiki hiyo tunapenda kuufahamisha umma kuwa habari nzima iliyoadikwa na gazeti hilo ni ya uongo na haina chembe ya ukweli.

Hata hivyo SBL inafahamu vema kwamba Uganda kupitia FUFA walialikwa na TFF na walijibu kwa maandishi kuwa hawawezi kuleta timu yao kwa sababu wanazozijua. Sasa hatuelewi maneno mengine yanatoka wapi. Ni wakati wa kupuuza uzushi wa namna hii wenye lengo la kuleta mtafuruku na kuvuruga uhusiano baina ya vyama vya mpira na wadhamini.

Mteja mmoja wa Vodacom kushinda shilingi milioni 100!!

Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania George Rwehumbiza akiongea na waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa Promosheni kubwa ya awamu ya pili ya Tuzo Milionea ambayo itamwezesha mteja kushinda shilingi Milioni 100 ,Droo itafanyika kwa muda wa wiki mbili kuanzia mwisho wa wiki hii(katikati)Meneja Matukio na Promosheni Rukia Mtingwa na kulia Meneja Mawasiliano Nector Foya.
Dar es Salaam, Januari 14.2010. Vodacom Tanzania imezindua awamu ya pili ya Promosheni yake kubwa ya Tuzo millionea ambayo itamuwezesha mteja mmoja wa Vodacom kushinda Sh. Milioni 100 taslim na wengine wengi kushinda zawadi kemkem.
Droo kubwa itafanyika mwezi Aprili mwaka huu.Mbali na mshinndi huyo pia wateja watapata nafasi ya kujishindia muda wa maongezi wenye thamani ya Sh. Milioni tisa.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkuu wa udhamini wa Vodacom Tanzania, George Rwehumbiza, alisema kupitia promesheni huyo, wateja saba wa Vodacom watajishindia muda wa maongezi wenye thamani ya shilingi 100,000 kupitia droo za kila wiki.
Droo zitafanyika kwa wiki 12 kuanzia sasa na hivyo wateja kujipatia muda wa maongezi wenye thamani ya shilingi milioni tisa.
Rwehumbiza alisema promosheni hiyo ni mwendelezo wa promosheni ya Tuzo milionea iliyoendeshwa na kampuni hiyo mwaka jana.
Mshindi wa Droo kubwa ya mwaka jana alikuwa ni Renatus Mkinga, Mkazi wa Mombasa, Ukonga Jijini Dar es Salaam, Mkinga alishinda shilingi milioni 100 na kuboresha maisha yake---alinunua gari na kujenga nyumba ya kisasa.
Aliishukuru Vodacom Tanzania kwa kuanzisha promosheni hiyo ambayo alisema hakika inasaidia kubadili maisha ya Watanzania kama ilivyosaidia kubadili maisha yake ambayo sasa yataboreka.
Mkinga ambaye ni mstaafu, aliwataka Watanzania kushiriki katika promosheni hiyo na kuachana na propaganda za kwamba washindi huwa wanapangwa.
“Tuache imani hizo potofu, mimi nimeshiriki mara nyingi katika promsheni hii na hatimaye Mungu akanisaidia nikawa mshindi, hivyo tushiriki kwa wingi ili tupate nafasi ya kushinda,” alisema wakati wa hafla ya kukabidhiwa zawadi yake ya fedha taslim Aprili mwaka jana,”
Rwehumbiza alisema promosheni hiyo ni kwa wateja wa akaunti za malipo ya kabla na baada.
Alifafanua kwamba mbali na droo za kila wiki pia kutakuwa na droo kubwa za kila mwezi ambazo zitawawezesha wateja wa Vodacom kushinda zawadi kem kem.
Ili kushiriki alisema mteja anajisajiri kwa kuandika neno milionea na kutuma kwenda namba 15588.
“Jinsi mteja anavyotuma mara nyingi ndivyo anavyojiweka kwenye nafasi kubwa ya kushinda,” alisema.
Alitoa wito kwa wateja wa Vodacom kuichangamkia promosheni hiyo kwani inalenga katika kuboresha maisha ya wateja wake.
“Promesheni hii inalenga kuboresha maisha ya wateja wetu lakini pia ni shukrani zetu za dhati kwa wateja wetu waaminifu kwa kutuwezesha kuwa mtandao unaoongoza Tanzania,” alibainisha.

SHUGHULI ZA UOKOAJI ZAENDELEA HAITI

Kwa siku ya pili mfululizo maelfu ya watu wamelala nje bila makao kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililotokea nchini Haiti.
Katika mji mkuu wa Port-au-Prince, wakaazi wanaendelea kuchimba vifusi ili kutafuta manusura na kufukua miili ya watu waliokufa. Miili iliyopatikana inawekwa barabarani huku ikiwa imefunikwa na mabati.
Kufikia sasa idadi kamili ya watu walioangamia bado haijulikani lakini rais wa Haiti, Rene Preval, amesema anaohofia ni maelfu ya watu.
Miongoni mwa waliouwawa ni askofu wa kanisa la Katoliki mjini humo, Joseph Serge Miot. Hospitali na mashirika ya kutoa misaada yanakabiliwa na changamoto kutokana na idadi kubwa ya majeruhi wanaohitaji matibabu.

Rais Kikwete awasili nchini Msumbiji!!

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mtoto Queen Kinguti(9) muda mfupi baada ya kuwasili jijini Maputo Msumbiji kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais Armando Guebuza kuendelea na muhula wa pili wa urais baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo mwezi Oktoba Mwaka jana.Queen ambaye wazazi wake ni wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji alikuwa miongoni mwa Watanzania waliojitokeza kumlaki Rais Kikwete na mkewe Mama Salma jana jioni.(picha na Freddy Maro)

Mtoto Queen Kinguti(kushoto) na Mwenzake Khalid Mgidos(kulia) wakiwakaribisha kwa maua Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete muda mfupi baada ya kuwasili jijini Maputo Msumbiji kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais Armando Guebuza kuendelea na muhula wa pili wa urais

Wadau wapanga mikakati ya kukabiliana na ugonjwa wa malae na ndorobo!!

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Kinga kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa JamiiDr. Geoffrey Kiangi (suti) akibadilishana mawazo na baadhi ya wadau kutoka sehemu mbalimbali waliohudhuria mkutano wa siku mbili wa Wadau wa kukabiliana na ugojwa wa Malale na Ndorobojijini jana. Mwengine ni Mratibu wa Taifa Mpango wa PATTEC ( Pan African Tsetse and Trypanosomosis Eradication Compaign )Joyce Daffa. ( Picha zote na Mwanakombo Jumaa -MAELEZO).

Kikundi cha maigizo ya sanaa cha Malachi nasau group cha jijini Dar kikiigiza kuhusu ugonjwa wa malale unaoambukizwa na ndorobo wakati waufunguzi mwa mkutano wa siku mbili wa wadau wa kukabiliana na ugonjwa wa malale na ndorobo jijini jana.

MKUU WA WACHAWI SASA AMPOKEA KRISTO!!

Kitabu hiki kimeandikwa na Mtume IYKE NATHAN UZORMA. Mtume Uzorma ni nabii mwenye nguvu, ambaye Bwana pia alimpaka mafuta katika roho kama Uashirio wa Agano la Mwisho. Kwa neema ya Mungu ya kipekee, Roho Mtakatifu amemtumia kwa namna nyingi mno katika kubadilisha maisha ya maelfu ya watu ambao hivi leo hushuhudia. Kitabu hiki kimechapishwa nchini Tanzania na Niim Computers & Graphics (T). Ukweli utakaoupata ndani ya kitabu hiki utayabadilisha maisha yako kabisa. Kushindwa na kuonewa na nguvu za giza kutakoma kabisa. Badala yake utakuwa mshindi na zaidi ya kushinda!
Ukweli utakaoupata ndani ya kitabu hiki utayabadilisha maisha yako kabisa. Kushindwa na kuonewa na nguvu za giza kutakoma kabisa. Badala yake utakuwa mshindi na zaidi ya kushinda!
Mwandishi ni msomi mwenye Shahada ya Udaktari wa Falsafa ya Metafizikia (Elimu ya kuchunguza chanzo cha uhai na maarifa) na kabla ya kukutana na Bwana, alikuwa ni Mkuu wa Kundi la Siri la Shetani litumikalo katika ulimwengu wa giza. Akiwa amezaliwa ukoo wa kichawi na kuishi kijiji ambacho ni cha wakazi wake wote ni wachawi, Mtume Uzorma alianza kutumika kichawi akiwa na umri wa miaka saba tu. Kutokana na elimu na ujasiri aliokuwa nao, haikuchukua muda mrefu kwake kupanda ngazi zote tano za kichawi na kufikiwa cheo cha Mkuu wa wachawi ambapo pia aliabudiwa kama mungu mdogo. Mtume Uzorma anashuhudia jinsi alivyokutana na nguvu kuu ya Yesu Kristo mwaka 1992 akiwa katika harakati zake kuvuruga kazi ya Mungu na kuwatesa watumishi wa Mungu, akiwa amepewa kibali na mamlaka na mungu wa ulimwengu huu ambaye ni Shetani mwenyewe.
Katika kitabu hiki Mwandishi anaelezea jinsi dunia yetu ya leo ilivyo katika mashambulizi makali ya nguvu za giza. Na kwamba watu ambao hawana imani ju ya nguvu ya damu ya Yesu, wapo katika hatari kubwa ya kuwa mateka wa nguvu za giza, bali wale ambao wanaamini katika Kristo wataweza kushinda muda wote kushinda vita hivyo.
SASA KINAPATIKANA MADUKA YOTE YA VITABU VYA KIKRISTO NCHINI.
KWA MAHITAJI AU TAARIFA ZAIDI, WASILIANA NA:
1. EFATHA BOOKSHOP (MWENGE DSM)
SIMU: 0754-684680, 0712-224104
2. NIIM MEDIA & PUBLISHING HOUSE (MAGOMENI DSM). SIMU: 0713-261425, 0754-527955, 0713-757051

Wednesday, January 13, 2010

MANJU MSITA ALETA UBUNIFU MPYA KATIKA MAVAZI YA HARUSI!!

Emmanuel na Diana wakikata keki siku ya harusi yao huku matron wao akiwaangalia.
Hatimaye mbunifu wa mavazi Manju Msita amefanikiwa kubuni mavazi kwa ajili ya maharusi. mavazi yaliyovaliwa kwa mara ya kwanza na maharusi Emmanuel na Diana hivi karibuni harusi iliyokuwa ya kupendeza na ya kuvutia iliyofanyika hapa jijini Dar es salaam.
Mavazi hayo ni kwa ajili ya maharusi wote pamoja na wasimamizi wa pamoja na watoto wanaotangulia mbele kwa ajili ya kupamba harusi, Manju Msita mbunifu wa mavazi mwandamizi hapa nchini anayefanya kazi zake katika katika kituo cha sanaa cha Mikono House kilichopo makutano ya barabara za Nyerere na Chang'ombe amesema tayari wanandoa hao wameshatumia nguo zake kwenye harusi yao, ilikuwa ni harusi nzuri na walifurahia nguo hizo.
Manju anaendelea kueleza kwamba awali maharusi hao walikuwa na mashaka kama nguo hizo zingewapendeza kutokana na mazoea ya maharusi wengi hapa nchini ambao wamekuwa wakivaa suti na magauni marefu, nguo ambazo zimeshonwa kwa tamaduni za kimagharibi zaidi, anaongeza kuwa hata hivyo wanandoa hao walikubaliana na wazo lake na aliwatengenezea nguo nzuri ambazo walizitumia kwenye harusi yao,
Ilikuwa ni harusi ya kusisimua kwani watu wengi hawajazoea kuona maharusi wakiwa wamevaa nguo za maharusi zilizotengenezwa na kurembwa kwa tamaduni za kiafrika na kila mtu aliyewaona maharusi hao alitamani awaangalie mara mbili.
Anasema nguo hizo zinatengenezwa kwa kitambaa cheupe laini na kigumu huku kikichanganywa na rangi nyeusi kiasi huku nguo hizo zikinakshiwa na marembo yenye mchanganyiko wa shanga na baadhi ya vitambaa vigumu.
Manju anasema harusi hiyo imemuongezea neema kwani mpaka sasa ana tenda ya kushona nguo za harusi zipatazo 10 kwa muda mfupi tu, kitu ambacho hakikuwepo hapo awali kwani oda nyingi zilikuwa ni nguo za kawaida, haya ni mabadiliko yanayokuja kwa kasi sana katika sanaa ya ubunifu wa mavazi na huenda watu wasipendelee tena kuvaa suti kweye harusi hivyo nawakaribisha kuja kujipatia ubunifu huu mpya wa nguo za harusi watu wote wanaopenda kutukuza Uafrika wao.

Rais Kikwete alipotembelea Majeruhi Pemba!

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma akimjulia hali mtoto Khamis Bakari(14) mkazi wa Wawi aliyelazwa kwenye hospitali ya Chake Pemba baada ya kujeruhiwa alipokuwa akijaribu kuingia katika uwanja wa michezo wa Gombani kuhudhuria maadhimisho ya sherehe za miaka 46 ya mapinduzi ya Zanzibar jana .Katika ajali hiyo mtu mmoja alipoteza maisha na wengine 18 kujeruhiwa na kulazwa katika hospitali hiyo ya chake ambapo Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Amani Abeid Karume na Waziri Kiongozi Shamsi Vuai Nahodha pamoja na viongozi wengine waliwatembelea majeruhi na kuwapa pole(picha na Freddy Maro)

Tuesday, January 12, 2010

MADEREVA UBUNGO WAMTIMUA KATIBU MKUU WAKE!

Kituo cha Mabasi yaendayo Mikoani- UBUNGO
Umoja wa Madereva wa Mabasi Tanzania (UWAMATA) umemvua madaraka Katibu Mkuu wake Ndg Salum Abdallah kwa tuhuma za kuhujumu mipango ya Serikali kuhakikisha kuwa madereva wa mabsi wanapata mikataba ya ajira, mishahara na posho kwa mujibu wa sheria za ajira. Hii inafuatia kitendo cha Katibu Mkuu huyu kuficha habari kuhusu maamuzi ya Serikali kuhusu ajira za madereva wa mabasi.
Uamuzi wa kumvua madaraka Katibu Mkuu ulichukuliwa hivi karibuni na Baraza la Wadhamini la UWAMATA, baada ya wajumbe wanne kati ya sita, akiwemo Mwenyekiti wa Taifa wa UWAMATA kuunga mkono pendekezo hilo.
Kwa muda mrefu madereva wa mabasi wamekuwa wakiilalamikia Serikali kuhusu kutokuwa na mikataba, kutolipwa mishahara, posho na maslahi mengine kwa mujibu wa Sheria ya Ajira na Mahusinao Kazini namba 6 ya 2004, kiasi cha kufikia hatua ya kuitisha mgomo tarehe 14 Agosti 2009, na hivi karibuni kuitishwa kwa mgomo mwingine tarehe 09 Januari 2010, ambao ulifutwa dakika za mwisho.
Mwenyekiti wa Barza la Wadhamini la UWAMATA Ndg Chrizant Kibogoyo amesema kuwa kumvua madaraka Katibu Mkuu ni moja ya harakati za kuhakikisha kuwa unakuwepo uwajibikaji wa hali ya juu katika kuhakiksha kuwa ajali za barabarani zinapungua kwa madereva kupatiwa maslahi yao ili wasipate visingizio vya kuendesha kwa mwendo wa kasi.
Hivyo kitendo alichofanya Katibu Mkuu huyu cha kutofikisha maamuzi ya Serikali kwa wanachama, ambao ni madereva wa mabasi ni cha hujuma kubwa. Vitendo kama hivi ndivyo husababisha madereva kuichukia Serikali bure wakati ambapo viongozi kama hawa ndio hukwamisha jitihada za Serikali kutokana na maslahi binafsi wayapatayo kutoka kwa baadh ya wamiliki wa mabasi wasiotaka kulipa mishahara na maslahi mengine kwa wafanyakazi wao (Madereva)

Asante
Chrizant Kibogoyo

Maadhimisho ya Miaka 46 ya mapainduzi ya Zanzibar yafana Gombani Pemba!!


Askari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama wakipita mbele ya jukwaa kuu kutoa heshima kwa Viongozi ambao walihudhuria katika sherehe za kutimiza miaka 46 ya Mapinduzi ya Zanzibar leo katika uwanja wa Gombani huko Pemba.Picha/Clarence Nanyaro….VPO


Wananchi mbalimbali kutoka vyama vya siasa vya CCM na CUF wakipita kwa maandamano katika kuadhimisha sherehe za miaka 46 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa Gombani huko Pemba .Wananchi wengi walijitokeza tofauti na miaka iliyopita kufuatia makubaliano ya amani ya hivi karibuni kati Rais Aman Karume wa CCM na Maali seif Sharif Hamad wa CUF.




RASHID MWEZINGO KUJA NA "HESHIMA YA NDOA"!

Wanamuziki wa bandi ya Msondo Rashid Mwezingo kushoto na Papa Upanga.

MWIMBAJI nyota wa muziki wa dansi nchini,Rashid Mwezingo 'Silver Boy' amesema anaipenda sana bendi ya msondo Music Band hivyo yupo mbioni kurejea katika kundi la ikiwa ikiwa ni baada ya wiki kadhaa za kuwa nje kutokana na matatizo ya kiutawala
'Mwezingo amesema muda mchache ujao atarejea kundini na kuanza kuonekana kama mwanzo baada ya kuweka sawa mambo yaliyokuwa yakimkabili ikiwemo ukweli juu ya jukumu walilonalo viongozi wa bendi ya msondo katika kulipa deni analodaiwa na benki ambapo alikopa kupitia udhamini wa TOT.Plus
Lakini nilipohamia Msondo uongozi wa TOT ukauandikia barua uongozi wa msondo kueleza kuwepo kwa deni hilo ambalo napaswa kulipa sh.67,000 kila mwezi alisema.
Alifafanua kuwa barua hiyo kwa kiasi fulani iliwachanganya viongozi wa Msondo ambapo walidhani jukumu la kulipa deni hilo ni lao, wakati ukweli ni kwamba ninapaswa kulipa mimi kupitia mshahara ninaolipwa kila mwezi.
Alisema badala yake viongozi hawo walisema hawawezi kumudu kulipa deni hilo hivyo kuamua kuachana nae, lakini baada ya kuwaelewesha bila shaka wameelewa na sasa yupo mbioni kulejea kundini na kuendelea kutoa burudani jukwaani na nimeshatunga kibao kitakachokwenda kwa jina la 'heshima ya ndoa' tutakachofanyia mazoezi baada ya kukaa pamoja hivyo kuwataka wapenzi wa Msondo kukaa mkao wa kushangweka

RAIS KARUME AZINDUA REDIO JAMII MICHEWENI PEMBA!!

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi mh. Aman Abeid Karume akifungua pazia kama ishara ya uzinduzi wa kituo cha Redio Jamii kilichopo Micheweni kilichojengwa kwa nguza za wananchi na Serikali pamoja na shirika la UNESCO katika kusherekea miaka 46 ya mapinduzi ya Zanzibar
Rais Karume akizungumza na mwakilishi wa UNESCO Bi. Vibele Jensen mara baada ya kuzindua kituo cha Redio Jamii kilichopo Micheweni kisiwani Pemba katika kuadhimisha miaka 46 ya mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika leo kisiwani humo. (Picha na Ramadhan Othman Pemba)


Monday, January 11, 2010

Makamu wa Rais atoa Msaada wa Baiskeli!!

=Katibu wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bwana Elisha Suleiman akimwelekeza jinsi ya kuendesha baiskeli ya miguu mitatu mlemavu wa viungo Rufiya Juma Khamis (15) wa Chokocho,Pemba muda mfupi baada ya kumkabidhi baiskeli hiyo ili iweze kumsaidia kuanza shule kutokana na kushindwa kufanya hivyo kwa sababu ya umbali kati ya nyumbani na shuleni. Wanaoshuhudia ni Wazazi wake Bwana Juma Khamis Idd na Bi Naima Bahari Juma. Baiskeli hiyo imetolewa msaada na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Dk Ali Mohamed Shein.
Picha/Clarence Nanyaro…VPO

MAANDALIZI YA KAMPENI YA KUTOKOMEZA MARALIA "ZINDUKA" YAENDELEA MOVENPICK!!

Kama unavyoona hii ni moja ya fulana zilizoandikwa ujumbe wa (ZINDIUKA) kampeni ya kutokomeza maralia ambayo itazinduliwa februari 13 kwa onyesho kubwa litakalofanyika kwenye viwanja vya Leaders Kionondoni huku mgeni wa heshima akiwa Rais Jakaya Kikwete, kampeni hiyo itaendeshwa karibu nchi nzima, pia kampeni hii ni kuhamasisha kizazi kipya cha vijana kupambana na ugonjwa wa maralia ili kuifanya jamii iliyo salama dhidi ya ugonjwa wa huo hapa nchini na inaratibiwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii pamoja na mradi wa kutokomeza maralia.
Baadhi ya wasanii wa muziki watakaopiga picha kwa ajili ya matangazo ya Redio, Telebisheni na Magazeti kwa ajili ya kampeni ya kutokomeza maralia nchini inayojulikana kama ZINDUKA wakiwa katika matayarisho hayo kwenye Hoteli ya Movenpick jijini Dar es salaam leo kutoka kulia ni Mfelo mpiga gitaa la bass kutoka B. Band, Taji Liundi mmoja wa wadau wanaoshughulikia kampeni hiyo, Marlow, Banana Zorro, Mpiga picha Raqey na Mwasiti.

mandalizi yakiendelea kwenye Hoteli ya Movenpick kwa ajili ya kupiga picha.
Hili ni eneo ambalo litatumika kupigia picha likitayarishwa


Hizi ni baadhi ya nguo zitakazovaliwa na wasanii wakati wa kupiga picha.

Mfurulizo wa matukio ya sherehe za Maadhimisho ya Mapinduzi ya zanzibar!!

Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein akikagua uimara wa vigae vilivyoezeka paa la jengo la Ofisi yake inayojengwa katika eneo la Tunguu huko huo Zanzibar katika maadhimisho ya Miaka 46 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Ofisi hiyo inategemewa kuimarisha shughuli za Muungano pindi itakapokamilika muda mfupi ujao. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mustafa Mohamed Ibrahim na Profesa Lekule wa Chuo cha Ardhi na usanifu wa Majengo.
Picha/Clarence Nanyaro…. VPO
Naibu Waziri wa Mawasiliano ,Sayansi na Teknolojia Dk Maua Abeid Daftari akijadiliana jambo na Mama Mwanamwema Shein,Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Ali Mohamed Shein,muda Mfupi baada ya Dk Shein kuweke jiwe la Msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari Makangale ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 46 ya mapinduzi ya Zanzibar

Goals galore as Angola kicks off




The CAF Africa Cup of Nations kicked off in the most dramatic fashion as Mali came back from four goals behind in the final quarter of an hour to share the spoils with hosts Angola in Sunday’s opening game.
It was a remarkable first-ever match at the brand new, and imposing, November 11 Stadium in Luanda, and the hosts looked to be on their way to an emphatic start to the 2010 finals in front of 50,000 cheering supporters.
But with their collapse at the end, the match fell one goal short of the Nations Cup record of nine goals in a single match set in 1963 when Egypt beat Nigeria 6-3 in Kumasi, Ghana.
ResultAngola 4-4 Mali
Goal of the dayAngola 4-3 Mali (Frederic Kanoute 87')Just three minutes were left in the game when Seydou Keita floated a long cross into the penalty box right onto the head of the lanky Kanoute. Just shy of the penalty spot, the 32-year-old striker climbed above the defenders and headed the ball into the back of the net with the same velocity as if it had been hit with the boot from close range. Defender Zuela made an effort to challenge Kanoute for the ball, but the determination of the former African Footballer of the Year left Angola’s goalkeeper with no chance to set up the dramatic finale.
Memorable moments Goalkeeper spillA needless spill by Angola’s new goalkeeper Carlos Fernandes from an innocuous looking corner set up the goalmouth melee from which Mali began their comeback. Several players had a swipe at the loose ball and the goalkeeper scrambled to recover, but it was Seydou Keita who forced it over the goalline. With 11 minutes left it seemed but a consolation strike, but in the end, it proved the turning point of a dramatic affair.
Flavio and Gilberto combinationAngola have not seen enough of the efficient partnership created over the years by Flavio and Gilberto. Injury in the main has kept them from recreating for their country what they had done season after season for Egyptian giants Al Ahly at club level. But Mali were witness to it when Gilberto floated in one of his left-footed crosses with characteristic pin-point accuracy, for Flavio to rise and head home a goal that put Angola into a 2-0 lead on the half-time whistle.

Sunday, January 10, 2010

Togo yajitoa mashindano ya CAN Angola

Mchezaji wa Togo Emmanuel Adebayor

Timu ya taifa ya Togo imejitoa kwenye michuano ya kombe la mataifa ya Afrika huko Angola baada ya tukio la kushambuliwa kwa risasi na kusababisha vifo.
Dereva wa basi, kocha msaidizi na afisa habari waliuawa. Wachezaji wawili waliuawa katika shambulio hilo lililotokea siku ya Ijumaa katika mkoa wa Cabinda.
Waandaaji wanasisitiza kuwa michuano itaendelea na kwamba wataimarisha usalama.
Lakini mchezaji wa Togo, Alaixys Romao, ameliambia gazeti moja la lugha ya kifaransa L'Equipe: "Tunazungumza na timu nyingine katika kundi letu kuzishawishi zisusie."
Katika mechi yao ya kwanza siku ya Jumatatu, Togo ilipangiwa kucheza na Ghana huko Cabinda na wachezaji wa timu hiyo inayojulikana kama Black Stars wamesema kuwa wako tayari kuendelea kucheza.
Ivory Coast na Burkina Faso ni timu nyingine zilizopangwa katika kundi B.

Saturday, January 9, 2010

Togo to play Africa Cup of Nations

Togo's national football squad have decided to participate in the Africa Cup of Nations in Angola, a day after their bus came under fire.The driver of the bus was killed and nine other people were wounded, including two players, in the attack, claimed by separatist fighters in Cabinda province. Al Jazeera's sports correspondent Mourad Laraba said the team confirmed their participation following a meeting with Angola officials.
"Yesterday African football federations had a meeting with the officials in Angola in order to ask them for guarantees to secure national team security in Cabinda, and we've just heard that the Togo national team will play in Cabinda," he said.
"The show will go on."
Authorities in Angola moved quickly to ensure they were doing everything possible to safeguard the tournament, which they insist will go ahead.
"We are going to further reinforce all the mechanisms and continue to guarantee security and create all the conditions which guarantee the success, and organisation and safety of poeple as planned," Goncalves Muandumba, Angola's minister for youth and sport, said.

Dr. Shein aweka jiwe la msingi ofisi ya mkuu wa mkoa Kaskazini Unguja kuadhimisha sherehe za Mapinduzi Zanzibar!!

Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein akiweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya sherehe za miaka 46 ya Mapinduzi ya Zanzibar, sherehe ambazo zitafanyika januari 12 Kisiwani Pemba.
Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein akijadiliana jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Seif Ali Idd muda mfupi baada ya Dk Shein kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya sherehe za mapinduzi Zanzibar.

Picha/Clarence Nanyaro

ML-8 -CLASSIC WEAR WAMWAGA MZIGO MPYA NENDA KAWAONE SASA!

Mali mpya imeingia kwenye duka la nguo la ML- 8-Classic Wear lililpopo Temeke Vetenary katika kituo cha mafuta cha Oil Com, kuna nguo za kike, Nguo za Kiume, Watoto, Viatu vya aina zote, Vipodozi Jezi za Timu mbalimbali barani Ulaya na vingine vingi Tembelea dukani hapo ili uweze kujipatia kilicho bora kwa mawasiliano zaidi piga simu namba 0773666080 au 0713-438055.












Togo weighs Africa cup withdrawal

Togo's national football squad is considering whether to withdraw from the Africa Cup of Nations in Angola after their bus came under fire.The driver of the bus was killed and nine other people were wounded, including two players, in the attack, claimed by separatist fighters in Cabinda province.
Emmanuel Adebayor, the Togo team captain, said that the squad would hold a meeting to discuss whether or not to stay for the tournament, seven matches of which are scheduled to be held in the region."I think a lot of players want to leave," he told BBC radio in Britain.
"They have seen one of their team-mates have a bullet in his body, who is crying, who is losing consciousness and everything." "I don't think they will be ready to give their life."Adebayor said that the team would only stay if their security coOrganisers have said that the tournament, which is due to kick off on Sunday, will go ahead, but African football officials will meet the Angolan government beforehand to seek assurances that players would be protected.Issa Hayatou, the president of the Confederation of African Football, will meet Paulo Kassoma, the prime minister, in Luanda, the capital on Saturday.
in depth
Organisers have said that the tournament, which is due to kick off on Sunday, will go ahead, but African football officials will meet the Angolan government beforehand to seek assurances that players would be protected.Issa Hayatou, the president of the Confederation of African Football, will meet Paulo Kassoma, the prime minister, in Luanda, the capital on Saturday.
They will meet to take decisions to guarantee the smooth running of the competition," a CAF statement said."The Confederation of African Football is terribly saddened by this event and express its total support as well as sympathy to the entire Togolese delegation."Al Jazeera's Andy Richardson, reporting from Luanda, said that he expected that players from most nations would be considering their participation despite the organisers' assurances."I think a lot of players involved here, a lot of clubs that they play for, and obviously their families back home are not as convinced as officials," he said."There are some multimillion-dollar players up there in Cabinda and a lot of them have clubs back in Europe who are obviously very concerned about them being exposed into an area where it seems security cannot be guaranteed."Cote d'Ivoire, Burkina Faso and Ghana were also to be based in Cabinda, which is separated from the rest of Angola by a slice of Democratic Republic of Congo, for the tournament. uld be guaranteed.

Friday, January 8, 2010

Hassan: Strong start is vital

Ahmed Hassan.

Ahmed Hassan has highlighted the importance of Egypt's opening CAF African Cup of Nations game against Nigeria, pointing out that it could be their benchmark for the remainder of the competition.
The Pharaohs, who will be bidding for their seventh continental crown and third in succession, begin their participation in the 10-31 January competition next Tuesday in Benguela.
They opened their victorious campaign two years ago with an emphatic 4-2 win over Cameroon, and Al-Ahly midfielder Hassan is keen for a repeat.
"Opening games are always very important," the captain said. "Our match against Nigeria will show how we will perform in the following matches, just like the 2008 tournament."
As for the strength of their west African opponents, Hassan added: "Nigeria are a strong team, but we are now familiar with all African teams."

PHOENIX ASSURANCE MAPINDUZI HOCKEY TOURNAMENT KUFANYIKA JANUARI 9-12/2010!!

Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Magongo Dar es salaam (DAR REGIONAL HOKEY ASSOCIATION) Bw. Savio Ferdinandus wakizungumza na waandishi wa habari leo kwenye ukumbi wa idara ya Habari Maelezo wakati akizungumzia mashindano ya kombe la Mapinduzi kwa mpira wa magongo Phoenix Assurance Mapinduzi Hockey Tournament yanayotalajiwa kuanza januari 9 mpaka 12 /2010 kwenye viwanja vya Jeshi Lugalo jijini Dare salaam.
Jumala ya timu 9 zitashiriki kutoka mikoa ya Dar es salaam , Arusha, Moshi Kilimanjaro na kutoka Zanzibar, timu hizo ni Magereza, TPDF, Dar Khalsa, Moshi Khalsa, Ngome Arusha Twigas, Kentucky, D.I. na Zanzibar
Mashindano hayo yanadhaminiwa na kampuni ya bima ya Phenex Assuranc ya jijini Dar es salaam ambapo kampuni hiyo imetoa shilingi milioni 5 kwa ajili ya matayarisho ya uwanja na vikombe pamoja na medali za dhahabu kwa timu zitakazoshinda kwenye michezo hiyo, mwingine anayeonekana kushoto kwenye picha ni Meneja mkuuu wa Phoenix Assurance of Tanzania Company Ltd Bw. S.C Wadhawan

VODACOM WAENDESHA PROMOSHENI YA (OFA BOMBA SAMSUNG)

Meneja Matukio na Promosheni wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa (katikati)akiwasiliana na mshindi wa Ofa Bomba Samsung Promosheni Mariam Andwele mkazi wa Ukonga temino one aliyejinyakulia shilingi Milioni 13,kushoto msimamizi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha Mrisho Milao na kulia ni Kaimu Mkuu wa biashara za rejareja wa Vodacom Upendo Richard.

Maeneo Hatari Kwa Usalama Wa Raia Jijini Dar

Kijitonyama, Sinza na Mikocheni:Mitaa ya Sayansi, Makumbusho na Maeneo ya Mikocheni Rose Garden nihatari sana kwa kina dada na kina kaka ambao huninginiza mabegi yalaptop na mapochi makwapani mwao.Kuna kundi la vijana linatumia magari kukwapua mabegi na mapochi hayo.Wanachofanya ni kwamba dereva anapunguza mwendo na kukusogelea kishaabiria aliokuwa nao hukwapua mikoba hiyo na kukimbia.Simu pia huibiwa kwa mtindo huo.Mbagala:Mitaa yote ya Mbagala Charambe, Hadi Kiburugwa hi hatari sana kwa kuwakuna kundi la vibaka linaloitwa Mbwa Mwitu.
Kundi hili hupora fedha,simu na kila ulichonacho hadi viatu. Ukikutana nao wanakushambulia kwavipisi vya nondo na kukuibia huku wakikuacha huna fahamu.Giraffe Hotel:Kwenye maegesho ya hoteli hii ni hatari sana kwa wenye tabia ya kuachamali za thamani ndani ya magari yao.Kuna kundi la vijana likishirikiana na walinzi wa hoteli hiyo, huvunjavioo vidogo ya nyuma sehemu ya kiti cha abiria, hung'oa power windowsna kuchukua kila wanachoweza.Hoteli imekuwa ikijibu wanaoibiwa kuwa hapa kwetu Parking is at ownersrisk.
Posta ya zamani na mpya:Maeneo haya ni hatari kwa wanaotumia daladala na wale wanaogeshamagari sehemu mbalimbali za katikati ya jiji hili. Watumia daladala waPosta huibiwa pesa na simu zao zilizomo kwenye mikoba na mifukoniwakati wakiwa wanagombania magari mida ambayo usafiri huwa mgumu.Wenye magari huibiwa vitu kama power windows na laptop ikiwa utaachandani ya gari. Na wezi wakubwa ni vijana wanaozagaa maeneo yamaegesho.
Bonde la Jangwani, Salenda Bridge na Bonde la Kigogo:Maeneo haya ni hatari kwani hamna makazi, hivyo vibaka hutumia mwanyahuo kufanya uhalifu mchana kweupe, na usiku maeneo haya ni hatarizaidi. Ukipata pancha maeneo ya jangwani nakushauri utembelee ringihadi eitha Faya au Magomeni Mapipa ambapo pana watu na pana usalama.
Vibaka hutokea kwa staili ya kukupa msaada na mwisho wa siku hukuachaukiwa huna kitu na huku gari yako ikiwa skrepa.Sea View, Ocean Road na Viwanja vya Golf Gymkhanna Club:Maeneo haya kuna vibaka hatari sana ambao hushambulia kwa kikundi nakupora mali zote na kukuacha ukiwa majeruhi. Maeneo haya yametuliasana na yanaonekana ni salama sana kwani yako jirani na ikulu, lakinihayana usalama wowote na ni hatari kabisa.
Usipite maeneo hayo kwa miguu mida ya kuanzia saa kumi na mbili nanusu giza likiwa linaingi, maana utakumbwa na dhahama.Daraja la Mlalakuwa, karibu na makao makuu JKT:Hapa watu wamesema weeeee wamechoka. Yaani watu wanavyoporwa kila sikukijua kikizama inaanza kuaminika kwamba wapiga loba ni askari wa hapoJKT ama wanashirikiana na hao vibaka. Wakazi wanajiuliza iweje sehemunyeti kama hiyo pawe na vibaka? Wanatokea wapi?
TUTAFIKA kweli?Afande Kova upooooooooo????

Uganda haitawanyonga Mashoga

Mswada mpya nchini Uganda unaotoa adhabu kali kwa wapenzi wa jinsia moja unatarajiwa kuondoa kipengele cha hukumu ya kifo dhidi ya watu hao.
Wabunge wa chama tawala hata hivyo wamesisitiza kwamba mswada huo ambao unapendekeza adhabu kali utawasilishwa mbele ya bunge hivi karibuni.
Baadhi ya nchi za magharibi zimepinga mswada huo ikiwemo Marekani.
Sweden imetishia kuondoa msaada kwa Uganda ikiwa mswada huo utaptishwa kuwa sheria. www.bbcswahili.com

Debo Band Sauti za Busara Festival Artists 2010!!

Debo Band is a nine piece Ethio-groove collective that has quickly earned an ever-growing and enthusiastic following in the USA performing for American, Ethiopian and Eritrean communities. Since 2006, Debo Band has been immersed in the unlikely confluence of traditional East African polyrhythms and pentatonic scales, classic American soul and funk music, and the instrumentation of Eastern European brass bands, which produced a unique form of dance music that Ethiopian audiences instantly recognise as the soundtrack of their youth, carried from party to kitchen on the ubiquitous cassette tapes of the time. Increasingly in the meantime, erudite American and European audiences are also getting hip to the Ethiopian groove, largely through CD reissues of classics on the Ethiopiques series.
With a unique instrumentation – including horns, strings, and accordion – that is a nod to the big bands of Haile Selassie's time, Debo Band is carrying the torch of classic Ethiopian music by giving new life to these old sounds. Their lead vocalist, Bruck Tesfaye, has the kind of pipes that reverberate with the sound of beloved Ethiopian vocalists like Mahmoud Ahmed and Alemayehu Eshete. But Debo Band is not content simply “covering” the older styles – they also perform original compositions and new arrangements of songs from modern and contemporary artists such as Teddy Afro and Roha Band. Their expansive repertoire and spirited performances have earned them respect and recognition, leading to invitations such as opening for concerts by the legendary Ethiopian greats Tilahun Gessesse and Getatchew Mekuria.
Danny Mekonnen, an Ethiopian-American jazz saxophonist and a PhD candidate in ethnomusicology at Harvard University, created Debo as a way of exploring the unique sounds that filled the dance clubs of “Swinging Addis” and as an outlet for experimenting with new arrangements, configurations, and compositional techniques. In addition to their dedication to Ethiopian music, the other members of Debo Band are involved in a huge array of musical projects, ranging from free jazz and experimental rock music to chamber and orchestral music. Band members have composed full orchestral works, scored silent films and documentaries, recorded albums with homemade electronic instruments, and for fun, study folk music traditions from around the world, including Balkan folk music, Balinese Gamelan, and Brazilian percussion ensembles.
For the last several months, Debo Band has committed itself to spreading its music to audiences far and wide. In early 2009 Debo toured the East Coast of USA, taking their Ethiopian grooves to diverse venues in New York, Philadelphia, and Washington DC. The band inspired all kinds of people to get up and dance, whether they had never seen iskista, the Ethiopian shoulder dance, or had been dancing it since childhood.
In May 2009, Debo travelled to Addis Ababa to perform at the 8th Ethiopian Music(s) Festival and several other locations throughout the Horn and East Africa. These performances affected Debo Band's creative and professional development in significant ways, particularly in the collaboration they began with several traditional musicians – vocalist Selamnesh Zemene, drummer Asrat Ayalew, and dancers Zinash Tsegaye and Melaku Belaye. All accomplished musicians in their own right, these musicians work together at Fendika, a leading azmari bet, or traditional music house, operated by Melaku in Addis Ababa. As will be seen at Sauti za Busara 2010, when working with these four musicians Debo Band grows into a forceful, energetic, and authoritative thirteen-piece ensemble capable of delightful, one-of-a-kind performances.
This engagement is supported by Mid Atlantic Arts Foundation through USArtists International with support from the National Endowment for the Arts and the Andrew W. Mellon Foundation.

Thursday, January 7, 2010

Mourinho lauds Inter's character

Inter Milan coach Jose Mourinho.

Inter Milan coach Jose Mourinho has given a thumbs-up to the job done by his players so far this season.
The four-time defending champions are cruising on top of Serie A and Wednesday's 1-0 win at Chievo saw Inter maintain an eight point cushion over Scudetto contenders AC Milan at the halfway point of the campaign. With I Nerazzurri unbeaten at the San Siro and having suffered only two defeats in 18 games, Mourinho has reason to be happy.
"I am extremely satisfied," said Mourinho. "My team is showing a lot of character and this is something that can only make a coach happy. I can talk about tactics and individual performances but at the end of the day, what makes the difference in games is the character displayed by the team. I have a lot of top professionals on the pitch and they do a great job."
My team is showing a lot of character and this is something that can only make a coach happy.
Jose Mourinho
If results go their way, Inter's lead could increase to 10 points this weekend. I Nerazzurri host rock-bottom Siena on Saturday while 24 hours later, Juventus take on in-form AC Milan in Turin in a battle for second spot.
I Rossoneri beat Genoa 5-2 in their first game of 2010 and are one point clear of Juve heading into Sunday's clash. Napoli host Sampdoria in buoyant mood after their 2-0 win at Atalanta in the last round extended their unbeaten run to 11 games and lifted the Partenopei to fourth.
A slip by Napoli could see Roma regain the fourth and last UEFA Champions League qualifying spot, provided the Giallorossi beat Chievo on Saturday. Genoa will be desperate to make amends for that hammering by Milan when they host relegation-threatened Catania on Sunday.
Fiorentina take on surprise package Bari looking to get back in the European qualification places. The Viola lie seventh after Wednesday's 5-1 triumph at Siena and are three points behind Napoli.
Bologna will be under pressure to beat Cagliari knowing that a defeat could see them drop to the relegation zone. The Rossoblu currently lie one point clear of 18th-place Catania.
Atalanta head into Sunday's game at Palermo looking for a new manager following Antonio Conte's resignation this week.
Conte stepped down after Wednesday's 2-0 defeat to Napoli that left the Bergamaschi in 19th position in the standings.
The Bergamo outfit have clinched just one win from their last eight matches.
Parma look to stop the rot when they travel to Leghorn to meet Livorno. Defeats to Roma and Juventus have seen Francesco Guidolin's side drop to sixth.
Strugglers Udinese will be hoping the presence of Serie A's top scorer Antonio Di Natale will inspire their team to return to winning ways against Lazio this weekend.
Di Natale missed the last two games through suspension and his absence hindered the Bianconeri, who lie just three points clear of the drop zone.

M-Net FACE OF AFRICA (EPISODE 11: THE REAL DEAL!

The Top 12 Face of Africa models face their toughest challenge yet on this week’s episode (Saturday 9 January at 19:00 CAT on M-Net) as they’re thrown into the deep
end of a high-fashion magazine editorial shoot and film a music video with Nigerian superstar D’Banj.
DStv audiences can tune in and watch as the safety net of Boot Camp has been removed – and the models need to show that they have what it takes to make it at the
highest level as they take part in a 14-page fashion editorial for South Africa’s Dossier magazine. Not only will they have to work under severe deadline pressure, but
they’ll also need to look their best while getting covered in paint from head to toe as part of the high-fashion concept of the shoot! One of the models learns
that sacrifices have to be made to make it in the fashion industry. Photographer and Editor Mia Ziervogel has high hopes for the Top 12 – but will they make the grade in
this world-class publication?
The models also face a second challenge – glamming it up in a high-tech music video for Nigerian hip hop star D’Banj – which premieres exclusively on this
week’s episode of Face of Africa. They’ll not only need to look good – but they need to do a little acting as well. As presenter Kaone Kario tells them, the
exposure they will gain from appearing in the video – set to be played on high rotation on music channels across the continent – is invaluable.
One of the models makes an error of judgment and learns a valuable career lesson as she is cut from the video altogether by D’Banj’s management.
What will the repercussions be for her, so close to the selection of the Top 10?
After surviving these two tough real-world challenges, the Top 12 still need to prepare for their appearance at Swahili Fashion Week. They’re also biding their time in the hope of realizing their wildest fashion dreams at the series finale in Lagos in February 2010 – but which ten models will make it that far?
The M-Net Face of Africa 2010 will walk away with a modeling contract from O Model Africa, USD 50 000 in cash from M-Net, skincare products for 12 months from Iman Cosmetics and a trip to New York, courtesy of Arise Magazine, to participate in New York Fashion Week. For more information and exclusive video from M-Net’s Face of Africa model search, log on to http://www.mnetafrica.com/ to find out more!

Chama cha wauguzi Tanzania chalaani kitindo cha kupigwa kwa muuguzi!!

Katibu mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii mama Blandina Nyoni.
Benjamin Sawe
Maelezo Dar es Salaam
Chama cha Wauguzi Tanzania (TANAA) kimelaani vikali kitendo cha kupigwa kwa Muuguzi Mkunga wa hospitali ya Tumbi Kibaa Bi Agness Msafiri alipokuwa katika harakati za kumhudumia mama mjamzito.
Katibu Mkuu wa chama hicho Romana Sanga alisema kitendo hicho ni kinyume cha sheria ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ni cha udhalilishaji kwa muuguzi husika ikiwa ni pamoja na taaluma kwa ujumla.
“Shambulio kama hili ni hatari kwa vile ingewezekana muuguzi huyu akapoteza maisha au kupata kilema cha kudumu”.Alisema bi Sanga.
Kutokana na shambulio hilo Bi Sanga ameiomba hospitali ya Tumbi Kibaha kuhakikisha sheria za kazi zinafuatwa ili haki iweze kutendeka.
Bi Sanga alisema kama hatua za kisheria hazitachukuliwa itasababisha vijana wenye nia nzuri ya kujiunga na fani hiyo kupoteza muelekeo kwa kuogopa kupigwa hivyo kupelekea kupungua kwa wataalamu wa kiuguzi kwa vizazi vijavyo.
Pia aliwaomba wauguzi wote nchini kuwa watulivu,waadilifu ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa upendo bila kuvunjwa moyo na kitendo cha kupigwa kwa muuguzi mwenzao
Hivi karibuni Bi Agness Msafiri alipigwa na Bwana James Msowoya ambaye ni mume wa mgonjwa akiwa katika harakati za kuokoa maisha ya mama mjamzito Bi Rebeca James.

Thomas Lubanga kujitetea Hague

Thomas Lubanga
Mawakili wa mbabe wa zamani wa kivita katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Thomas Lubanga hii leo watawasilisha hoja zao mbele ya mahakama ya uhalifu wa kivita huko the Hague Uholanzi.
Lubanga anatuhumiwa kuwasajili watoto wadogo kama wapiganaji wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo mwaka 2007.
Kesi hiyo iliyoanzishwa mwaka jana ndiyo ya kwanza ya uhalifu wa kivita kufunguliwa mbele ya mahakama ya ICC.

TIMU YA WABUNGE YAPOKEA VIFAA VYA MICHEZO KUTOKA SBL!!

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Mh. Joel Bendera akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo wakati alipokabidhiwa vifaa vya michezo na Kampuni ya Bia ya Serengeti leo asubuhi kwa ajili ya timu ya mpira wa miguu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano la Tanzania inayokabiliwa na mchezo mkali utakaofanyika kati yake na timu ya Baraza la wawakilishi la Serikali ya Mpinduzi ya Zanzibar januari 12 mjini Zanzibar kabla ya mchezo wa fainali katika mashindano ya kombe la Muungano linaloendelea mjini humo katika kuadhimisha sikukuu ya Mapinduzi,
Timu hiyo yenye wachezaji 25 tayari imeshawasili mjini Zanzibar kujiandaa na mchezo huo huku ikiwa na mfungaji wake mahiri Mh.Abdull Mwinyi ambaye ni Mbuge wa bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania.
Waziri Bendera amekabidhiwa Jezi 25 na Bukta zake Soksi 25 viatu pea 25 mipira 5 vikombe viwili na zawadi nyingine nyingi, Bendera pia ameitaka timu ya waandishi wa habari ya TASWA FC kujiandaa kwa ajili ya kukutana nao kwani wabunge hao wako tayari kucheza na waandishi wa habari wakati wowote na wataifunga tu timu hiyo ya TASWA FC, wengine waliopo katika picha ni Teddy Mapunda Meneja Uhusiaon wa Kampuni ya Bia Serengeti katikati na mwisho ni Brand Manager wa kampuni hiyo Nandi Mwiyombela.
Waziri Joel Bendera akipokea vifaa hivyo kutoka kwa Teddy Mapunda meneja uhusiano wa SBL na Mwisho aliyeshika viatu na mpira ni Brand Manager wa kampuni hiyo Nandi Mwiyombela.

Wednesday, January 6, 2010

RAIS JAKAYA AMFAGILIA DIDIER DROGBA NA TIMU YA IVORY COAST!!

Rais Jatkaya Kikwete akiongea na timu za taifa za Tanzania, Ivory Coast na Rwanda wakati wa chakula cha mchana kilichoandaliwa kwa ajili ya timu hizo leo kwenye hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa mpira wa miguu rais amewashukuru viongozi wa shirikisho la soka la Ivory Coast kwa kukubali mwaliko wa kuja Tanzania, na amesema watanzania watawaombea wakati wote watakapokuwa nchini Angola kwenye michuano ya Kombe la Mataifa Huru ya Afrika yanayotarajiwa kuanza jumapili ijayo Ivory Coast itacheza mchezo mwingine wa kirafiki kesho kwenye uwanja wa Taifa na timu ya Rwanda baada ya kuifunga Taifa Stars goli 1-0 katika mchezo uliopita uliofanyika januari 4 kwenye uwanja huohuo na inatarajia kuondoka keshokutwa kuelekea Angola.
Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi jezi mchezaji ya timu ya taifa ya Tanzania mchezaji Dider Drogba jezi hiyo imeandikwa jina lake Mgongoni.

Rais akiwakatika picha ya pamoja na wachezaji wa wa Timu ya Ivory Coast.

Rais akiwa na wachezaji wa timu ya Timu Taifa ya Rwanda.

Meneja matukio wa Serengeti Breweriers Bahati Singh naye akila shavu na akina Didier Drogba
Rais Jakaya akimsikiliza Kocha wa timu ya Taifa Marcio Maximo wakati alipokuwa akizungumza na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Joel Bendera kwenye chakula cha mchana kilichoandaliwa kwenye Hoteli ya Golden Tulip kwa timu za taifa za Ivory Coast, Rwanda na Tanzania kulia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini Adam Malima.

Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania leo mara baada ya chakula cha mchana.

MVUA YASABABISHA HASARA MBEZI BEACH USIKU WA KUMKIA LEO!!

Gari aina ya Toyota saloon likiwa limezolewa na maji maeneo ya Mbezi Beach Karibu na njia panda ya kwenda White Sands Hotel kutokana na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo jijini Dar es salaam picha zimetumwa na mdau Bahati Singh meneja matukio na promosheni wa Kampuni ya Bia Serengeti

Katika mti huu kuna gari aina ya Toyota Landcruiser lililofunikwa na mti huu baada ya kudondokewa kutokana na upepo ulioambatana na mvua kubwa wakati lilipokuwa likipita maeneo hayo usiku wa kuamkia leo maeneo ya Mbezi Beach matukio haya yalipatikana asubuhi na kuchukuliwa na mdau Bahati Singh