Monday, January 25, 2010


Nimekuwa katika vuguvugu la habari na mawasiliano kwa njia ya blog kwa muda sasa.Kila siku huwa napitia blogs zaidi ya 500! Huwa natumia huduma ya www.bloglines.com. Ukiandika kitu basi naambiwa umeandika na hivyo napita na kusoma.Ukiwa hujaandika,basi siku hiyo napata muda wa kuperuzi au kutafuta blogs zingine,kuziingiza kwenye orodha yangu ya bloglines.Siku inakuwa imekwenda au naendelea na kazi zingine.
Leo nikiwa katika pitia pitia yangu mtandaoni,nimekutana na blog ya Madaraka Nyerere,mtoto wa Hayati Baba wa Taifa,Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Cha kwanza kilichonijia kichwani ni hasira fulani.Iweje siku zote hizi sikujua kuhusu blog ya Madaraka? Haikutangazwa au ilikuwaje? Hasira zangu ziliyeyuka kama vile barafu inapopigwa na jua baada ya kuanza kuipitia blog yake.Imesheheni habari kemkem.Madaraka ni mwandishi mzuri.Simulizi zake ni nyepesi kama pamba lakini maudhui yake ni mazito kuliko yale mawe yanaouzunguka mji wa Mwanza.
Bonyeza hapa ili kuitembelea blog hiyo. Nikisema mkaribishe nitakuwa nakosea kwani amekuwepo kwa muda sasa.Bravo Madaraka.
Pichani juu ni Madaraka Nyerere(kulia) akiwa na Jaffar Amin,mtoto wa Iddi Amini aliyewahi kuwa Rais wa Uganda. Soma zaidi kuhusu mkutano wao.

KanumbaFront 

Katika siku kama ya leo,miaka 26 iliyopita pale mkoani Shinyanga, alizaliwa kijana na kupewa jina la Steven. Hivi leo ni maarufu kama Steven Kanumba au kama mwenyewe anavyojiita wakati mwingine “The Great”. Kwa maana hiyo,leo ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Steven Charles Kanumba.Happy Birthday!

Kwa mtu yeyote ambaye anafuatilia maendeleo ya tasnia ya filamu nchini Tanzania,bila shaka atakubaliana na mimi nikisema kwamba Kanumba ni miongoni mwa waigizaji wa filamu(Film Actors) ambao ni maarufu zaidi nchini Tanzania. Leo hii ni vigumu kuiongelea sanaa ya filamu nchini bila kumhusisha Kanumba kwa njia moja ama nyingine.

Kwa hivyo,haishangazi sana kuona kwamba,katika mwaka uliopita jina lake lilikuwa takribani la kudumu katika vyombo mbalimbali vya habari vikiwemo vya mtandaoni,mitaani nk. Bila shaka unakumbuka jinsi habari ya Kiingereza Vs Kiswahili ilivyozua mjadala wa kitaifa. Kila mtu akasema lake.

Baada ya mambo kama yale,mijadala kama ile,watu hupenda kujua what next? Nilimtafuta Steven Kanumba ili kujua machache kuhusu mipango yake ya mwaka huu.

Unajua Kanumba angependa kupata chakula cha mchana (lunch) na actors gani maarufu hapa ulimwenguni? Una habari kwamba katika Curriculum Vitae(CV) yake ameongeza cheo cha “Blogger”? Unajua ana malengo gani mwaka huu? Una habari kwamba Kanumba hivi sasa amedhamiria kuibua vipaji vingine katika ulimwengu wa uigizaji filamu? Fuatana nami;

BC: Mpaka sasa unalionaje soko la filamu nchini Tanzania? Kumekuwa na mabadiliko gani ya kimsingi ukilinganisha toka ulipoanza mpaka hivi leo?

SK: Soko limetanuka kiasi kwamba tunatambulika kimataifa. Pia hivi sasa makampuni ya kusambaza kazi zetu yameongezea ikiwemo na pesa kwa kiasi fulani tofauti na hapo mwanzo.Safari bado ni ndefu lakini angalau inatia moyo.
BC: Mwaka 2009 ndio tumeumaliza.Jina lako liligonga vyombo vya habari kwa mambo kadha wa kadha.Unaweza kusema umejifunza mambo gani katika mwaka ulioisha? (more…)

Model-Taji
Sitaki kusema mengi leo.Kama unapenda unachokiona pichani basi mtembelee Master Taji Liundi katika blog yake ya u-modo kwa kubonyeza hapa.
Ukitaka kusoma mahojiano yangu na Taji Liundi(Master T) hivi karibuni,bonyeza hapa.

summit-logo
Je wewe ni mwanablogu (Blogger) au mdau wa habari na mawasiliano kwa umma kwa kutumia mtandao? Kama jibu ni ndio, tafadhali unaombwa kujiorodhesha kwa ajili ya maandalizi ya Kongamano Maalumu la Kitaifa kwa ajili Wanablogu (Bloggers) na wadau wa habari na mawasiliano wa Tanzania (Tanzanians Bloggers Summit) linalotarajiwa kufanyika Desemba mwaka huu jijini Dar-es-salaam,Tanzania.
Dhumuni la kongamano hili ni Kuelimishana, Kufahamiana, Kuamsha Utambuzi Rasmi Kuhusu Tekinolojia ya Blogu na Mawasiliano ya Umma kwa Kutumia Mitandao, Kusaidia Utambuzi Rasmi juu ya mchango wa blogu nchini Tanzania kama chombo muhimu cha habari na mawasiliano, Kuelimishana jinsi gani blogu zinaweza kutumika katika kuleta maendeleo katika nyanja za kijamii, kisiasa na kiuchumi, kuburudisha, kukuza utamaduni nk.
Wataalamu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wataalikwa kutoa mada na mafunzo mbalimbali kuhusiana na tekinolojia ya kublogu, zana nyinginezo za mawasiliano mtandaoni kama vile mitandao jamii(social networking), online forums nk.Kutakuwa na vipindi vya maswali na majibu.
Ili kufanikisha maandalizi ya Kongamano hili la kihistoria, kujiorodhesha kwako ni muhimu sana. Muda wa kujiodhoresha ni kuanzia tarehe 12/8/2009 (Jumatano) mpaka 12/9/2009 (Jumamosi) tu.

Kinachohitajika ili kujiandikisha ni :

Jina Lako, Anuani yako ya barua pepe (E-mail), Mahali Ulipo au unapoishi (Nchi,mji nk),Namba ya Simu (sio lazima) na Anuani au URL(Universal Resource Locator) ya blogu yako (mfano www.kongamano.blogspot.com/wordpress.com/.com/typepad nk). Vyeti vya Ushiriki vitatolewa kulingana na habari utakazoziorodhesha hapa.

Unaweza kujiorodhesha kwa kutuma ombi lako kwa barua pepe kwenda; summit@bongocelebrity.com.

Zingatia tarehe za kujiandikisha.

Ni mwezi mmoja tu! Asante kwa ushirikiano. UMOJA NI NGUVU!

nyerere1
Hayati Baba wa Taifa,Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na mkewe Mama Maria Nyerere wakiwa wameongozana kuelekea kwenye mojawapo ya dhifa za kitaifa enzi hizo.
Picha hii inatoka pale Mtaa Kwa Mtaa. Mtembelee kwa kubonyeza hapa.
summit-logo
Je wewe ni mwanablogu (Blogger) au mdau wa habari na mawasiliano kwa umma kwa kutumia mtandao? Kama jibu ni ndio, tafadhali unaombwa kujiorodhesha kwa ajili ya maandalizi ya Kongamano Maalumu la Kitaifa kwa ajili Wanablogu (Bloggers) na wadau wa habari na mawasiliano wa Tanzania (Tanzanians Bloggers Summit) linalotarajiwa kufanyika Desemba mwaka huu jijini Dar-es-salaam,Tanzania.
Dhumuni la kongamano hili ni Kuelimishana, Kufahamiana, Kuamsha Utambuzi Rasmi Kuhusu Tekinolojia ya Blogu na Mawasiliano ya Umma kwa Kutumia Mitandao, Kusaidia Utambuzi Rasmi juu ya mchango wa blogu nchini Tanzania kama chombo muhimu cha habari na mawasiliano, Kuelimishana jinsi gani blogu zinaweza kutumika katika kuleta maendeleo katika nyanja za kijamii, kisiasa na kiuchumi, kuburudisha, kukuza utamaduni nk.
Wataalamu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wataalikwa kutoa mada na mafunzo mbalimbali kuhusiana na tekinolojia ya kublogu, zana nyinginezo za mawasiliano mtandaoni kama vile mitandao jamii(social networking), online forums nk.Kutakuwa na vipindi vya maswali na majibu.
Ili kufanikisha maandalizi ya Kongamano hili la kihistoria, kujiorodhesha kwako ni muhimu sana. Muda wa kujiodhoresha ni kuanzia tarehe 12/8/2009 (Jumatano) mpaka 12/9/2009 (Jumamosi) tu.

Kinachohitajika ili kujiandikisha ni :

Jina Lako, Anuani yako ya barua pepe (E-mail), Mahali Ulipo au unapoishi (Nchi,mji nk),Namba ya Simu (sio lazima) na Anuani au URL(Universal Resource Locator) ya blogu yako (mfano www.kongamano.blogspot.com/wordpress.com/.com/typepad nk). Vyeti vya Ushiriki vitatolewa kulingana na habari utakazoziorodhesha hapa.

Unaweza kujiorodhesha kwa kutuma ombi lako kwa barua pepe kwenda; summit@bongocelebrity.com.

Zingatia tarehe za kujiandikisha.

Ni mwezi mmoja tu! Asante kwa ushirikiano. UMOJA NI NGUVU!

dinabc
Unamjua Dina Marios kama mtangazaji maarufu wa Clouds FM kupitia kipindi chake cha Leo Tena. Ambacho unaweza kuwa hukijui kuhusu Dina ni kwamba yeye pia ni blogger. Dina ana-blog kupitia www.dinamarios.blogspot.com. Ninachopenda kuhusu blog ya Dina ni topics mbalimbali ambazo anazirusha kila mara.Mtembelee ujionee mwenyewe kwa kubonyeza hapa.

ansbert-ngurumobcJina la Ansbert Ngurumo sio geni hata kidogo miongoni mwa wapenda habari na mawasiliano na hususani wapenzi wa habari za magazetini. Ansbert ni miongoni mwa waandishi wa habari mahiri nchini Tanzania ambao wamejijengea sifa na heshima kutokana na kazi zao za uandishi wa habari.

Safu yake ya Maswali Magumu,inayochapishwa katika gazeti la Tanzania Daima kila jumapili inabakia kuwa safu yenye wasomaji lukuki huku kila mara ikizua mijadala ya aina yake jambo ambalo ni uthibitisho kwamba sio tu inapendwa bali pia hujibu na pia kuuliza Maswali Magumu.

Ansbert ni blogger mzoefu pia.Blog yake ambayo inaongozwa na kichwa cha habari, Utakapojua Hujui Ndipo Utakapojua, ni sehemu mojawapo nzuri ambapo unaweza kukuta kazi zake za uandishi,mitizamo na pia mikingamo.

Hivi karibuni,jamaa wa mtandao wa Rap21,walifanya naye mahojiano ambayo kwa kila hali ni “must read” kwa mtu yeyote ambaye yupo kwenye fani ya ku-blog au ni mfuatiliaji wa maendeleo ya tekinolojia hii ambayo mimi naiita mapinduzi ya karne katika ulimwengu wa habari na mawasiliano.

Katika mahojiano hayo,Ansbert ameongelea kwa mapana jinsi ambavyo blogs,ikiwemo ya kwake, zinazidi kuboresha mapinduzi hayo na pia jinsi gani blogs zinaweza kutumika katika kuboresha maisha ya wanajamii,kutunza historia zetu,kufichua maovu nk.Bonyeza hapa ili kusoma mahojiano hayo.


tk-bannerbc
Kwa mujibu wa jamaa wa Technorati,inakadiriwa kwamba blog mpya zaidi ya mbili huanzishwa katika kila sekunde,kila siku.Mpaka tarehe 31 Julai mwaka 2006 kulikuwa tayari na blog zaidi ya milioni 50!

Pamoja na mafanikio hayo ya uandishi huu unaoitwa uandishi wa kiraia (Citizen Journalism) ,bado hakuna takwimu za uhakika zinazoonyesha ni blogs ngapi “zinakufa” kila siku au kutelekezwa.Lakini ni wazi kwamba ni nyingi pengine kupita kiasi.Mtu anaanza kublog kwa kasi ya aina yake.Baada ya siku chache haonekani tena hewani.Amekosa muda au amekosa hamasa.Lengo alilokuwa nalo limempotea. Hawezi tena.Kila mtu ana majibu yake.

Ndio maana inapotokea mtu akadumisha blog yake kwa angalau mwaka mmoja inasemekana hawezi kuacha tena ku-blog.Kimsingi mtu huyo anastahili sio tu pongezi bali heshima.

Mmojawapo miongoni mwa watu hao ni mwanadada anayeonekana pichani hapo juu.Kwa wengi anajulikana kama TK lakini jina lake halisi ni Teddy Kalonga.TK ni miongoni mwa watu wanaotambulika kirahisi nchini kwetu ambao hawajabaki nyuma kunako tekinolojia hii ya blog.Hivi majuzi alisheherekea mwaka mzima tangu aanzishe blog yake inayopatikana kwa kubonyeza hapa.

Tunaungana na wengine wote kumpongeza TK na kumtakia kila la kheri katika kuendeleza “libeneke” kama anavyopenda kusema mwanablogu mwingine maarufu,Muhidini Issa Michuzi.Bonyeza hapa uone jinsi Teddy alivyosheherekea mwaka wake mmoja wa ku-blog.Hongera.

NB: Kama na wewe una blog yako na unasheherekea mwaka au miaka,usisite kuujulisha umma kupitia hapa hapa ndani ya BC.

pawasabc
Mchezaji maarufu aliyewahi kuichezea Simba Sports Club, APR ya Rwanda na ambaye kwa sasa alikuwa akiichezea timu ya Azam FC Club inayoshiriki ligi ya Vodacom Boniface Pawasa (Baba Ubaya ) amejiunga na Chuo Cha Biashara (CBE) cha jijini Dar-es-salaam mwezi mmoja uliopita ili kuongeza elimu.

Akizungumza na blog ya Full Shangwe hivi karibuni,Pawasa amesema kwa sasa umri wake umeenda hivyo anahitaji kutengeneza maisha mapya na yenye malengo ya baadae na ndiyo maana ameamua kufuata nyayo za wachezaji wenzake waliopita kwa kujiendeleza kielimu.

Pawasa amesema kwa sasa anasomea mambo ya utawala wa biashara ambapo atakuwa chuoni hapo kwa mwaka mmoja akisomea cheti katika fani ya utawala wa biashara yaani Business Administration. Pawasa pia amesema akimaliza anatarajia kuendelea na elimu yake ya Diploma mpaka atakapokamata digrii yake ya kwanza hapo ndiyo ataangalia afanye nini.

Pawasa amesema kuwa pamoja na kwamba kocha wa timu yake ya Azam Santos anamuhitaji ili arejee kundini kuipigania timu yake katika mzunguko wa pili wa ligi ya Vodacom hataweza kurejea tena kwa sababu pia ana maumivu ya misuli ambayo yatamchukua muda mrefu kupona hivyo ameona asipoteze muda kusubiri apone wakati anaweza kufanya kitu kingine cha maendeleo.

Amewashukuru wachezaji wenzake kwa kumpokea chuoni hapo na anasema kwa sasa anafurahia sana maisha ya chuoni kwani rafiki zake wa karibu Ally Mayay, Aron Nyanda na Wilfred Kidilu wamempokea na wanampa sapoti ya hali ya juu na kama wao wameweza kwa nini yeye ashindwe “najua nitaweza tu na nitasoma kama nilivyojiwekea malengo yangu” anamaliza Baba Ubaya.

Pichani juu Boniface Pawasa a.k.a Baba Ubaya(kulia) akiwa na mwenyeji wake na Rais wa serikali ya wanafunzi wa Chuo cha Biashara (CBE) Bw. Ally Mayay ambaye aliwahi kuwa mchezaji wa Yanga.

Habari na picha kwa hisani ya John Bukuku anayeendesha blog ya Full Shangwe.Mtembelee.

No comments:

Post a Comment